Dereva wa
lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo Septemba 09,2014,
amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida.
Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa.
Mmoja wa
mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka
anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu
waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.
|
No comments:
Post a Comment