MAENDELEO:-Hii ndio Sarafu ya Shilingi Mia Tano ambayo Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuitoa October 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 08, 2014

MAENDELEO:-Hii ndio Sarafu ya Shilingi Mia Tano ambayo Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuitoa October 2014.


Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kutoa toleo jipya la sarafu ya Sh. 500, inayotarajiwa kuingizwa kwenye mzunguko na kutumika rasmi kama fedha halali nchini, kuanzia mwezi ujao wa Octoba 2014.

Hatua hiyo imechukuliwa na BoT kwa kuzingatia sababu mbalimbali, ikiwamo noti ya Sh. 500 iliyopo sasa kwenye mzunguko kupita kwenye mikono ya watu wengi katika kipindi cha muda mfupi na hivyo, kuchakaa haraka.

Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki wa BoT, Bw.Emmanuel Boaz, aliwaambia waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana  Septemba 07,2014,kuwa sarafu hiyo itakuwa ikitumika sambamba na noti zilizopo za Sh. 500 mpaka hapo noti hizo zitakapokwisha katika mzunguko.


Alitaja sababu nyingine iliyozingatiwa katika kutoa sarafu hiyo kuwa ni noti hizo (za Sh. 500) kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe zinapokuwa zimefikia ukomo wake.

Sababu nyingine ni sarafu kuwa na uwezo wa kukaa kwenye mzunguko kwa miaka mingi (zaidi ya miaka 20) zaidi kuliko noti.

Alisema sarafu hiyo ina umbo la duara lenye michirizi pembezoni, kipenyo cha milimita 27.5 na uzito wa gramu 9.5, ina rangi ya fedha na imetengezwa kwa madini aina ya chuma na “Nickel”.

Pia upande wake wa mbele ina sura ya Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Sheikh Abeid Aman Karume, na kwa nyuma ina taswira ya mnyama nyati akiwa mbugani.

Vilevile, ina alama maalumu ya usalama iitwayo “latent image”, iliyopo upande wa nyuma, ambayo ni kivuli kilichojificha, ambacho huonesha thamani ya sarafu “500” au neno BoT inapogeuzwageuzwa.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad