PASHA PASHA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015:-Simba SC yaangukia pua kwa URA ya Uganda ikikubali kichapo cha bao 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 12, 2014

PASHA PASHA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015:-Simba SC yaangukia pua kwa URA ya Uganda ikikubali kichapo cha bao 1-0.

Kiungo mshambuliaji wa Simba Amri Kiemba akijaribu kuwatoka mabeki wa URA, wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu hizo uliochezwa jioni ya leo Septemba 12,2014, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Katika mchezo huo Simba SC imefungwa bao 1-0 lililofungwa na Kalanda Frank katika dakika ya 42.

Ligi Kuu Tanzania bara 2014/2015 inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu na Mbeya City watafungua dimba na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine siku hiyo.

Mabingwa watetezi, Azam FC watafungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakati washindi wa pili
Yanga SC wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo.

Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC. 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad