Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar .
Nao Ndanda
FC imeonyesha imepania kufanya kweli, baada ya kuichapa Stand United kwa mabao
4-1.
Ikiwa ndiyo
mechi ya kwanza kwa timu hizo ya Ligi Kuu Bara, Stand ikiwa nyumbani Kambarage
imelala kwa mabao hayo 4-1.
Wageni
Ndanda walipata mabao yao kupitia Paul Ngalema, Nassor Kapama na Ernest Mwalupani.
Wakati
wenyeji ambao walijitahidi kurekebisha mambo walipata bao la kufutia machozi
kupitia kwa Salum Kamana.
Mechi
ilikuwa nzuri nay a kuvutia lakini wageni ndiyo walioonyesha soka la kuvutia
zaidi.
Maafande wa JKT Ruvu wameonyesha kweli walipania kuanza ligi kwa kishindo
baada ya kuishika nyumbani timu ya Mbeya
City.
Katika mechi
hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine, kila timu upande ulionyesha soka
la kuvutia, lakini mwisho hakuna aliyeona nyavu za mwenzake.
Kipindi cha
kwanza kilikuwa na mashambulizi ya zamu lakini kipindi cha pili, Mbeya City
wakabadilika na kuanza kushambulia sana.
Wachezaji
wake, Deus Kaseke, Mwagane Yeya na Themi Felix walionekana kupania kushinda
lakini mambo yalikuwa magumu.
Kiungo Jabir
Aziz alionyesha kuwapa wakati mgumu Mbeya City akishirikiana na washambuliaji
Realiants Lusajo na Iddi Mbaga.
Hadi mwisho,
Mbeya City ambao walishika nafasi ya kwanza msimu uliopita, walikuwa hawajapata
kitu na wageni wao hali kadhalika.
Ruvu
Shooting imeanza ligi vizuri kwa kuwatungua maafande wa Magereza, Prisons kwa
mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandini, Pwani, wenyeji
ndiyo walikuwa sawa zaidi.
Vijana wa David Mwamwaja walijitahidi kusawazisha mabao hayo katika kipindi cha
pili, lakini wapi.
Jumapili,
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam itakuwepo Mechi ya ‘Wapwa’ wakati Simba
itakapocheza na Coastal Union.
LIGI KUU
VODACOM RATIBA
Septemba
21,2014.
Simba v
Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Septemba
27,2014.
Simba v
Polisi Moro [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar
v Ndanda FC [Manungu, Morogoro]
Azam FC v
Ruvu Shooting [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mbeya City v
Coastal Union [Sokoine, Mbeya]
Mgambo JKT v
Stand United [Mkwakwani, Tanga]
Septemba
28,2014.
JKT Ruvu v
Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
Yanga v
Prisons [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
|
No comments:
Post a Comment