Nao Manchester United,
wakicheza Ugenini King Power Stadium, wamechapwa Bao 5-3 katika Mechi ambayo
waliongoza kwa Bao 3-1 lakini maamuzi utata ya Refa Mark Clattenburg kutoa
Penati 2 kwa Leicester na ulinzi hafifu uliwapa ushindi wa chee Leicester City.
Man United walimaliza Mechi
hii wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao Chipukizi Tyler Blackett kupewa Kadi
Nyekundu Dakika ya 82 na Refa Mark Clattenburg kutoa Penati ambayo Leonardo
Ulloa alifunga Bao la 5.
Man United, wakiwa wanaongoza
3-1, Refa Clattenburg aliwapa Leicester City Penati ya ajabu baada ya Rafael
kusukumwa na Vardy na Refa huyo kupeta na walipoingia ndani ya Boksi Mchezaji
huyo akajiangusha na Refa huyo kutoa Penati ambayo Leicester walifunga Bao lao
la Pili.
Dakika mbili baada Mkongwe
Cambiasso akaisawazishia Leicester na Gemu kuwa 3-3 na kuanzia hapo kila kitu
kikaenda sawa kwao na kupewa Penati nyingine.
BPL-LIGI KUU ENGLAND 2014/2015 - RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 27,2014.
1445 Liverpool v Everton
1700 Chelsea v Aston Villa
1700 Crystal Palace v
Leicester
1700 Hull v Man City
1700 Man United v West Ham
1700 Southampton v QPR
1700 Sunderland v Swansea
1930 Arsenal v Tottenham
Jumapili Septemba 28,2014.
1800 West Brom v Burnley
Jumatatu Septemba 29
2200 Stoke v Newcastle
|
No comments:
Post a Comment