|
Golikipa wa Polisi Morogoro,
Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa
Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo September 27,2014.
Timu ya soka ya Simba SC
imelazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
baada ya jioni hii Septemba 27,2014,kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Hiyo ni sare ya pili
mfululizo kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya wiki iliyopita kutoka 2-2
na Coastal Union Uwanja wa Taifa, licha ya kuongoza 2-0 hadi mapumziko.
|
|
Mshambuliaji wa Simba,
Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati wa mchezo wa Ligi
Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro uliofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ramadhani Singano 'Messi'
Hadi mapumziko, tayari Simba
SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi dakika
ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Timu ya Polisi inayofundishwa
na Mohammed ‘Adoph’ Rishard ilibadilika na kuanza kusukuma mashambulizi langoni
mwa Simba SC ambapo Danny Mrwanda, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC,
aliisawazishia Polisi baada ya kumzidi mbio na maarifa beki Joseph Owino kabla
ya kumchambua vizuri kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’.
|
Azam FC imepata ushindi wake
wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo
kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam FC ambao walianza ligi
kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 3-1, imeshinda mabao hayo mawili leo, yote
yakitupiwa kimiani na Mrundi, Didier Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne.
Matokeo mengine ya Ligi Kuu Vodacom
2014/2015 ni kama ifuatavyo:-
Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar 3 – 1 Ndanda FC
Mbeya City 1 – 0 Coast Union
Mgambo Shooting 0 – 1 Stendi
United
Karibu
kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana
/Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment