LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Tazama Picha na Matokeo ya mechi za Leo September 27, 2014 huku Kadi nyekundu kwa Rooney kumkosesha Mechi 3 za Timu yake dhidi ya Everton,West Brom na Chelsea. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Saturday, September 27, 2014

demo-image

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Tazama Picha na Matokeo ya mechi za Leo September 27, 2014 huku Kadi nyekundu kwa Rooney kumkosesha Mechi 3 za Timu yake dhidi ya Everton,West Brom na Chelsea.

.com/simgad/
_77863454_costa
Vinara wa Ligi Kuu Uingereza 2014/2015- Chelsea Leo September 27, 2014,wakicheza kwao Stamford Bridge wameitandika Aston Villa Bao 3-0 na kuzidi kupaa kileleni kwa kufikisha Pointi 16 sasa.

 Hadi Mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Oscar la Dakika ya 7 huku Dakika ya 59 Diego Costa aliipa Chelsea Bao la Pili kwa Kichwa na Willian aliipa Chelsea Bao la 3 katika Dakika ya 79 baada ya Shuti la Diego Costa kuokolewa na Kipa Guzan na kumkuta Willian.
1411822828465_wps_20_LIVERPOOL_ENGLAND_SEPTEMB
Aidha Bao la Dakika ya 91 la Sentahafu Phil Jagielka likawapa Everton Sare ya Bao 1-1 walipocheza Mechi ya Merseyside Uwanjani Anfield na Watani zao Liverpool katika mchezo wa Ligi kuu Uingereza 2014/2015 leo Septemba 27,2014.
1411824549275_Image_galleryImage_LIVERPOOL_ENGLAND_SEPTEMB
Liverpool walifunga Bao lao katika Dakika ya 65 kwa Shuti safi la Nahodha wao Steven Gerrard.

Huku Anfield ikisheherekea ushindi dhidi ya Mahasimu wao na Dakika zikiyoyoma Krosi ya Aiden McGeady iliokolewa kwa Kichwa na Mpira kumkuta Phil Jagielka na kufumua Shuti safi sana kutoka Mita 30 na kufanya Gemu imalizike 1-1.

1411828530592_lc_galleryImage_MANCHESTER_ENGLAND_SEPTEM
Wakicheza kwao Old Trafford, Manchester United wameifunga West Ham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kukwea hadi Nafasi ya 7 lakini watamkosa Nahodha wao Wayne Rooney kwa Mechi 3 zijazo baada ya kutwangwa Kadi Nyekundu.

Hadi Mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Nahodha Wayne Rooney, ambae sasa ametimiza Miaka 10 akiwa Old Trafford,  baada kuunganisha pande safi la Rafael katika Dakika ya 5 na Robin van Persie kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 22 baada ya kazi njema ya Ander Herrera na Radamel Falcao.

West Ham walifunga Goli lao baada ya kutokea kizaazaa kufuatia Kona na Diafra Salho kukwamisha Mpira wavuni katika Dakika ya 37.
1411831405418_lc_galleryImage_27_September_2014_Barclay
Dakika ya 54 Man United walibakia Mtu 10 baada ya Refa Lee Mason kumpa Kadi Nyekundu Nahodha Wayne Rooney kwa madai amemchezea Rafu mbaya Stewart Downing.

Hii inamaanisha Rooney atazikosa Mechi 3 za Timu yake dhidi ya Everton,West Brom na Chelsea.

1411822631282_wps_12_Everton_s_Kevin_Mirallas_

1411833819015_Image_galleryImage_HULL_ENGLAND_SEPTEMBER_27
Zabaleta kulia akimpongeza lampard baada ya kufunga bao la nne ,ambapo Mabingwa watetezi Manchester City imeshinda mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Hull City katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Uingereza jioni ya leo September 27, 2014.

Mabao ya City yamefungwa na Sergio Aguero dakika ya saba, Edin Dzeko dakika ya 11 na 68 na Frank Lampard dakika ya 87, wakati mabao ya Hull yamefungwa na Eliaquim Mangala aliyejifunga dakika ya 21 na Hernandez kwa penalti dakika ya 32.
1979531_498061360331331_7050042709637302485_n
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp call_skype_logo+255789925630.

As It Stands Tables EPL 2014/2015.

Pos.TeamPGDPts
1 61216
2 6713
3 6511
4 6410
5 6210
6 6-310
7 628
8 618
9 608
10 6-18
11 607
12 6-17
13 6-26
14 6-26
15 6-15
16 5-15
17 5-45
18 6-94
19 5-33
20 5-63

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *