LIGI KUU ENGLAND 2014/2015:-Matokeo yote ya Mechi za Leo September 13,2014 huku Diego Costa akipiga 3-Chelsea ikishinda 4-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 13, 2014

LIGI KUU ENGLAND 2014/2015:-Matokeo yote ya Mechi za Leo September 13,2014 huku Diego Costa akipiga 3-Chelsea ikishinda 4-2.

Goli la dakika ya 83 la Martin Demichelis limeinusuru Manchester City kulala mbele ya Arsenal baada ya kupata sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza leo Septemba 13,2014 jioni.

Sergio Aguero alitangulia kuifungia City dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri ya Jesus Navas kabla ya Jack Wilshere kuisawazishia Arsenal kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Aaron Ramsey.

Alexis Sanchez akaifungia Arsenal bao la pili dakika ya 74 kabla ya Debuchy kuisawaishia City. Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck alikaribia kufunga dakika ya 11 baada ya kugongesha mwamba, wakati kiungo mpya wa Man City, Frank Lampard alionyeshwa kadi ya njano.

Mchezaji Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Arsenal .

Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Manchester City .


Jumamosi Septemba 13,2014.

Arsenal 2 - 2 Man City 

Chelsea 4 – 2 Swansea 

Crystal Palace 0 – 0 Burnley 

Southampton 4 – 0 Newcastle 

Stoke 0 – 1  Leicester 

Sunderland 2 – 2 Tottenham 

West Brom 0 – 2 Everton

EPL 2014/2015-LIGI KUU UINGEREZA-RATIBA.
**Saa za Bongo.

Jumapili Septemba 14,2014

1800 Man United v QPR

Jumatatu Septemba 15,2014

2200 Hull v West Ham
Nao Chelsea walitoka nyuma kwa Bao 1-0 Uwanjani kwao Stamford Bridge na kuifunga Swansea City Bao 4-2 huku Straika wao hatari Diego Costa akipiga Hetitriki.

Bao la 4 la Chelsea lilifungwa na Straika wao mpya Loic Remy alieanzia Benchi na hii ikiwa ni Mechi yake ya kwanza.
Chelsea walianza kwa mkosi baada ya Nahodha wao John Terry kujifunga mwenyewe katika Dakika ya 11 akiwa kwenye harakati za kuokoa lakini walisawazisha Dakika ya 45 baada ya Kona kuunganishwa kwa Kichwa na Diego Costa.

Bao la Pili la Swansea lilifungwa na Jonjo Shelvey.
MSIMAMO EPL 2014/2015.

NAFASI
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
4
9
12
2
Swansea
4
3
9
3
Southampton
4
5
7
4
Man City
4
3
7
5
Tottenham
4
2
7
6
Aston Villa
3
2
7
7
Liverpool
3
2
6
8
Arsenal
4
1
6
9
Everton
4
-1
5
10
Leicester
4
-1
5
11
Hull
3
0
4
12
Stoke
4
-1
4
13
Sunderland
4
-1
3
14
West Ham
3
-1
3
15
QPR
3
-4
3
16
Man United
3
-1
2
17
Crystal Palace
4
-3
2
18
Burnley
4
-3
2
19
West Brom
4
-5
2
20
Newcastle
4
-6
2

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad