“Mfano mheshimiwa Sitta alitoa tamko lake kuwa
hadhi ya bunge maalum la katiba ipo juu kidogo ya tume ya mabadiliko ya katiba
ni upotoshaji wa makusudi wakati iko wazi kuwa vyombo hivyo viwili viko sawa
kabisa, labda anataka kuonyesha kuwa yuko juu ya jaji Warioba”alisema mh
Kibamba.
Aidha
amesema kuwa mwenyekiti huyo mh Sitta ameamua kuendelea na bunge maalum la
katiba huku akijua wazi kuwa upatikanaji wa katiba mpya haupo huku akiwa ni kinara
wa kuwaaminisha watanzania kuwa katiba mpya itapatikana hata kama hakuna
ushiriki wa UKAWA,wala Waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar na Mwanasheria
mkuu wa Zanzibar,ambao nao wamejitoa katika mchakato huo.
Akimzungumzia
mwanasheria mkuu wa Tanzania jaji FREDRICK WEREMA amesema kuwa jaji huyo
amekuwa bingwa wa kutoa tafsiri tata ambapo aliwahi kushauri kuwa tafsiri ya
siku 70 ya bunge hilo ni pamoja na siku za mapumziko na sikukuu ndipo wabunge
walianza kufanya kazi hadi siku za jumamosi na baadae alitoa tafsiri tofauti
tena ambayo imewafanya wabunge kutofanya kazi siku za mapumziko.
“mh WEREMA
amekuwa mshauri mbaya wa viongozi wa bunge hilo akiwaminisha mambo ambayo siyo,
ambapo amewashauri kuwa mchakato wa katiba unaweza kukamilika bila hata ya
wajumbe waliotoka nje,ndugu werema amekuwa akishauri pia muundo wa serikali
tatu ulio katika rasimu unaweza kubadilika kirahisi tu jambo ambalo linapingwa
na wanasheria wengi”amesema mwenyekiti wa JUKATA.
Akizungumzia
maamuzi ambayo JUKUTA wamechukua kuhusu viongozi , KIBAMBA amesema kuwa
viongozi hao kutokana na makosa yao wameamua kuwatangaza rasim kuwa maadui
wapya wa katiba mpya ambapo wamesema kuwa wanapendekeza kuwa wasifikiriwe
kupewa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya nchi hii kwa miaka kumi ili
wapate nafasi ya kujifikiri na kujitathmini.
Aidha katika
hatua nyingine JUKATA wamemtaka mwenyekiti wa bunge maalum la katiba
kusitisha mara moja bunge hilo ambapo wametao wiki mbili na kama
halitasitishwa wao kama JUKATA kwa wingi wao wataelekea mjini Dodoma
wakiwa na makufuki kwa ajili ya kulifunga wenyewe.
|
No comments:
Post a Comment