Nje Kidogo
ya Stand kuu ya Mabasi wilayani Ngara mkoani Kagera na ni Basi la Nyehunge
linalofanya safari zake kati ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera na Jiji la
Mwanza.
Wasafiri wanaotumia
vyombo vya kubeba abiria mkoani Kagera wametakiwa kudai haki zao zinazopaswa
kutolewa wakati wakiwa safarini na kujitokeza kutoa taarifa pale panapojitokeza
kuwepo mazingira ya unyanyasaji wakati wa safari.
Ushauri huo
umetolewa na Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya kuthibiti vyombo vya Usafiri wa
majini na nchi kavu (SUMATRA) mkoa wa Kagera, Kapten Alex Katama,wakati
akizungumzia juu ya mamlaka hiyo ilivyojipanga kukabiliana na changamoto mkoani
Kagera.
Kapteni
Katama amekiri kuwepo changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa abiria
wakiwa ndani ya vyombo vya usafiri,ingawa taarifa dhidi ya changamoto hizo
zimekuwa hazitoshelezi kutokana na baadhi ya watu kutozipa umuhimu na
kuzifikisha kwenye ofisi za mamlaka ili zitafutiwe ufumbuzi.
Ametaja
mojawapo ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara ni abiria
kuzidishiwa nauli pamoja na matumizi mabaya ya lugha,hata hivyo taarifa za
changamoto hizi zimekuwa hazifikishwi katika ofisi za mamlaka.
Pamoja na
matatizo haya kuendelea kujitokeza miongoni mwa abiria,Mamlaka imekuwa
ikiendelea kutoa ushauri kwa watu wote watumiao usafiri wa abiria,kuhakikisha
wanatambua haki zao na kujitokeza kufika ofisi za mamlaka kutoa taarifa pale
haki hizo zinaposhindwa kutolewa.
|
No comments:
Post a Comment