Haya mabasi
yaligongana katikati ya daraja lakini hizi picha nilipiga baada ya kukuta
yameshasogezwa kutoka eneo yalipogongania.
|
Waliosimama
kwenye hii picha wako juu ya gari ambalo ndilo liligongwa na basi la J4
darajani na kutumbukia, ndani yake wamefariki Daktari wa hospitali ya mkoa wa
Mara na mume wake.
|
Shuhuda
Patrick ambae ni mwandishi wa habari amesema taarifa alizozipata ni kwamba
Wafanyakazi wote wa mabasi haya kuanzia dereva mpaka kondakta wamefariki.
|
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe
(Picha na Maktaba).
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya J4
Express na Mwanza Coach yafungiwe mara moja.
Akizungumza
na mwandishi wa habari mjini Musoma Jana September 06,2014, Dk Mwakayembe amesema sehemu
iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu 39 na wengine zaidi ya 70
kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva alikuwa akimuona mwenzake, hivyo
ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
“Ile sehemu
ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na daraja lipo katikati,
kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na uzembe kama huu unasikitisha
sana. Walikuwa wanaonana na hata lile gari dogo walikuwa wanaliona… hii hali
inasikitisha sana,” alisema Dk. Mkwakyembe.
Alitahadharisa
kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali ya kizembe ataaamuru
vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya wananchi.
“Katika uongozi wangu
madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe
mara moja wakisababisha ajali za kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.
Waziri wa uchukuzi, Mhe Harrison Mwakyembe
amefanya maamuzi kadhaa, kupunguza ajali za barabarani. Ifuatayo ni kauli yake:-
1.
Tunaanza
na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi
pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4
na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa
tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa
lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi
lazima anipishe’ .
2.
Tumeelekeza
Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile
tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na
watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii
mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi
kila mwezi’
3.
Nimeagiza
lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari
ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive
haendeshi mtu gari kuchukua abiria.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
|
No comments:
Post a Comment