UHALIFU BUKOMBE:-Jeshi la Polisi Tanzania Latangaza zawadi ya shilingi millioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa Majambazi na Silaha zilizoibiwa kituo cha Polisi wilaya ya Bukombe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 06, 2014

UHALIFU BUKOMBE:-Jeshi la Polisi Tanzania Latangaza zawadi ya shilingi millioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa Majambazi na Silaha zilizoibiwa kituo cha Polisi wilaya ya Bukombe.


Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi wilaya ya bukombe na kuua askali polisi wawili na kujeruhi askali wengine wawili.

 Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Ernest Mangu amesema majambazi hao walivamia kituoni hapo saa nane usiku wa September 06,2014,ambapo walirusha mabomu na kuua Askali wawili, waliouwawa ni  WP. 7106 Uria Mwandiga  na G. 2615 Dastani Kimati waliojeruhiwa ni H.627 Mohamedi Hassani na CPL. 5131 David  Ngupama.

IGP.Mangu amesema katika uvamizi huo silaha mbalimbali zimeibiwa ambapo Jeshi la Polisi limetangaza zawadi ya shilingi millioni kumi kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao na silaha zilizoibiwa.

Akithibitisha kupokelewa kwa majeruhi na miili ya marehemu,Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe ,Daktari Honaratha Rutatinsibwa amesema hali za majeruhi ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya rufaa Bugando.
 UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.

 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad