TATIZO LA KUJINYONGA DUNIANI:-Tanzania iko katika nafasi ya Pili barani Afrika huku Duniani ni ya 8 kwa kujiua. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 07, 2014

TATIZO LA KUJINYONGA DUNIANI:-Tanzania iko katika nafasi ya Pili barani Afrika huku Duniani ni ya 8 kwa kujiua.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limetowa ripoti yake inayosema kwamba idadi ya watu wanaojiua duniani imeongezeka na kufikia kiwango cha kutisha.

 Ripoti inasema kwamba katika kila sekunde 40 mtu mmoja anajiua.

Shirika hilo limelitaja tatizo hilo kama la kiafya ambalo linahitaji kushughulikiwa baada ya kufanya utafiti wake katika nchi 172 duniani.

Wastani wa dunia wa watu kujiua upo kwa watu 11.4 kwa kila watu 100,000 huku wanaume kama wanawake kwa idadi sawa wakijaribu kujiua.

Nchi ambazo zinaongoza kwa vifo vya kujiua ni Guyana (asilimia 44.2 kwa kila watu 100,000), ikifuatiwa na Korea Kaskazini na Korea Kusini (asilimia 38.5 na 28.9 kwa kila 100,000).
 Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dk Margaret Chan.

Nchi nyingine ni Sri Lanka (28.8), Lithuania (28.2), Suriname (27.8), Msumbiji (27.4), Nepal na Tanzania (24.9 kila mmoja), Burundi (23.1), India (21.1) na Afrika Kusini (19.8). 

Nchi nyingine ni za Russia na Uganda (zote zikiwa na wastani wa 19.5), Hungary (19.1), Japan (18.5) na Belarus (18.3).

Katika nchi zenye kipato kikubwa matatizo ya afya ya akili kama msongo wa mawazo umeelezwa kusababisha asilimia 90 ya vifo vya kujiua ukilinganisha na asilimia 60 katika nchi za Asia kama China na India, WHO imesema.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kwamba ni lengo ifikapo mwaka 2020 kuhakikisha kwamba wanapunguza wastani wa kujiua kwa asilimia 10.

Hata hivyo, utafiti umeonesha kuna changamoto kubwa kutokana na vifo hivyo kutokea katika makundi ambayo yanaonekana kutengwa, wengi wao wakiwa masikini, wenye matatizo mbalimbali na wanaoishi katika hali ya kutothaminiwa au kukubalika katika jamii.

Magonjwa ya kuambukiza Utafiti umeonesha kwamba nchi zenye pato dogo ambazo zinahangaika kuwatimizia wananchi wake mahitaji muhimu yakiwemo ya afya, kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza wana wakati mgumu wa kutambua na kuwasaidia watu wanaotaka kujiua.

Akizungumzia utafiti huo , Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba alisema ni jukumu la wizara yake kuhakikisha amani katika familia inadumishwa.

Alisema kujiua ni kosa la jinai na pia ni dhambi, hivyo wizara yake inahamasisha upendo ndani ya familia kuwepo na mazungumzo ili kuepuka matatizo yanayosababisha watu kujiua.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad