UHALIFU:-Raia wa Vietnam akamatwa na mzigo mkubwa wa meno ya tembo na kucha za Simba Wenye Thamani ya Mil 189,420,000. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 01, 2014

UHALIFU:-Raia wa Vietnam akamatwa na mzigo mkubwa wa meno ya tembo na kucha za Simba Wenye Thamani ya Mil 189,420,000.

Jeshi la Polisi linamshikilia  Raia wa  Vietnam Dong Van(47) kwa kumkamata akiwa na meno 65 na kucha 447 za Simba kinyume cha sheria vyenye thamani ya Shilingi Milioni 189,420,000.


Kamishna Msaidizi  wa Polisi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  Hamisi Selemani, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana wakati alipotaka kusafirisha nyara hizo kwa kutumia Shirika la Ndege la Qatar Airways kwenda nchini Vietnam kupitia Doha.

Amesema alipopekuliwa alikutwa na nyara hizo ambazo alizihifadhi kwenye

pakiti 7 za kahawa na pakiti moja ya mchele  na kuzichanganya na pakiti nyingine 15 za vyakula vya aina mbalimbali

Kamanda Selemani amesema  pakiti hizo ziliwekwa ndani ya begi la nguo ili kupoteza ushahidi wa aina ya mzigo alioubeba kwa wakaguzi wa uwanjani hapo.

Aidha amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

Habari Na:- Times Fm.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad