UMOJA wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), umemtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kuacha
kuwaingilia kwenye mambo kwa vile hayamhusu.
Kauli ya Ukawa imekuja siku moja
baada ya Zitto kusema hana uhakika na wala haamini kama umoja huo utakuwa
endelevu hadi uchaguzi mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya
upinzani kuungana kisha kugawanyika.
Alisema siku zote Watanzania wanapenda kuwa
na upinzani imara ambao watu wanaweka maslahi yao pembeni na kuungana dhidi ya
chama kilichopo madarakani.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana(Julai 31,2014),
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa,
alisema haoni umuhimu wa kujibizana na mtu aliye nje ya umoja huo kwa sababu
hawezi kujua dhumuni la kuungana.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
“Hatuhitaji kuumiza kichwa
wala kujibizana na mtu aliye nje ya Ukawa, kwa sababu hajui ulianzishwa kwa
lengo gani, atabaki kutabiri kitu ambacho hana uhakika nacho, bali anazungumza
kutokana na matakwa yake.
“Kwanza si msemaji wa Ukawa,
tunashangaa hata kukaa na kuanza kujadili suala lisilomhusu, ni nani na ninyi
waandishi wa habari mnapaswa kumuuliza maswali wakati akizungumza hayo,”
alisema Dk. Slaa.
Alisema Ukawa haufanyi kazi
kwa kufuata maneno ya barabarani, bali wanafanya kazi kwa vitendo, ikiwa ni
pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi nini wanataka ili waweze kuyafanyia
kazi.
Alisema tangu kuanzishwa kwa
umoja huo, wamekwenda zaidi ya mikoa 17 na majimbo yake ili kusikiliza maoni ya
wananchi ambayo wameyachukua na kuyafanyia kazi, hivyo basi hawana muda wa
kukaa na kujadili kauli za watu zinazotolewa barabarani za kujadili masuala
yasiyowahusu.
“Sisi tunafanya kazi na
Watanzania, hatufanyi kazi na mtu mmoja mmoja, ndiyo maana tulikwenda mikoa 17
na majimbo yake kwa ajili ya kuwaelezea umoja wetu na mikakati tuliyopanga
ndani ya umoja huu, hivyo basi hatuna nafasi ya kujadili kauli ya mmoja mmoja,”
alisema.
Alisema kutokana na hali
hiyo, viongozi wa umoja huo hawawezi kuishi kwa imani, bali wanafanya kazi kwa
vitendo ili wananchi waweze kuwahukumu katika uchaguzi ujao.
Alisema Ukawa haupo kwa ajili
ya Katiba peke yake, bali ni kuangalia maslahi ya wananchi katika nyanja
mbalimbali za kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha wanaondokana na hali ngumu ya
maisha na kupata mafanikio.
Alisema mkakati uliopo ni
kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa kwa vitendo ili wananchi wenyewe waweze
kuwanyooshea vidole kwenye chaguzi zijazo.
Naye Katibu wa Ukawa ndani ya
Bunge, Julius Mtatiro, alisema mawazo ya mtu yanapaswa kuheshimiwa, lakini
umoja huo hauwezi kufanya kazi ya utabiri kama utaendelea au kuvunjika.
“Ukawa hauwezi kufanya kazi
ya utabiri, kwa sababu tulipoungana tulikuwa na malengo ya dhati, ikiwa ni pamoja
na kuondoa tofauti zetu na kuangalia maslahi ya wananchi na si kauli ya mmoja
mmoja, japo naheshimu mawazo yake,” alisema Mtatiro.
Mtatiro alitolea mfano kwa
kusema kauli ya Zitto ni sawa na falsafa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo
wamekuwa wakitangaza kila kona kuwa upinzani Tanzania unaelekea kufa wakati si
kweli.
WAJUMBE
Katika hatua nyingine, Ofisi
ya Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba imewataka wajumbe wa Bunge hilo kuwasili
Dodoma Agosti kwa ajili ya kuanza mkutano huo kama ulivyopangwa.
Taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari mjini Dar es Salaam na ofisi hiyo, ilisema Bunge Maalumu la
Katiba linatarajia kuanza vikao vyake Agosti 5, mwaka huu mjini Dodoma.
Taarifa hiyo ilisema Agosti 4
itakuwa siku maalumu kwa ajili ya mambo ya kiutawala, hivyo wajumbe wote
wanapaswa kufika Ofisi za Bunge Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi.
|
Friday, August 01, 2014
SOMA:-UKAWA Wamshukia Mbunge Zitto Kabwa.’’
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment