WHO imesema
mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa Ebola ni wa kihistoria kutokana na kasi ya kuenea
na idadi ya watu waliopoteza maisha.Mlipuko huo ambao hadi sasa umeua zaidi ya
watu 1,427 Magharibi mwa Afrika.
Juzi,Agosti
25,2014, Waziri wa Afya DRC,Bw. Felix Kabange Numbi alikaririwa akisema Ugonjwa
wa Ebola umeingia nchini humo na watu wawili walioambukizwa, wamefariki dunia
katika Jimbo la Ikweta, Kaskazini Magharibi wa nchi hiyo.
Taarifa hizo zimeendelea kuwashtua na
kuwafanya Majirani kuzingatia tahadhari ambapo mkuu wa mkoa wa Kigoma,Bw. Issa
Machibya amesema ‘pamoja na tishio la ugonjwa huu kwamba uko DRC Congo lakini
DRC ya mbali sana kule kaskazini wanakopakana na Afrika ya kati na Sudan,
tumeanza kuchukua tahadhari kwenye mipaka yetu manake binadamu wanatembea na
maingiliano ni makubwa’.
‘Kuanzia leo
Agosti 27,2014,Bw.Machibya amesema nimemuagiza katibu tawala wa mkoa magari
yote yenye uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu wamesharudi
nyumbani yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo licha ya
kuweka vipeperushi’ .
Bw.John
Ndunguru ambae ni Katibu Tawala wa mkoa amesema ‘Kwenye hospitali zetu
wameshatenga chumba maalum kama atatokea mgonjwa yeyote manake inabidi Wagonjwa
hawa wawekewe kinga au wigo kwa siku 48, vilevile wizara ya Afya imeahidi
kutuletea vifaa vya kutosha hasa vya kinga na dawa mbalimbali, tayari maafisa
Afya wako hata uwanja wa ndege kukagua kila anaeingia’.
Aidha Tayari
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatarajia kufunga vifaa vya kupimia joto
(Thermal Scanner) katika mipaka ya nchi ili kudhibiti kuenea ugonjwa wa ebola
ambao umeelezwa umeingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
DRC inakuwa
nchi ya tano barani Afrika kukumbwa ingawa nchi hiyo kwa mara ya kwanza
ilikumbwa na ugonjwa huo mwaka 1976 kabla ya kuingia Uganda mwaka 2012.
Nchi
nyingine za Afrika zilizokumbwa na ugonjwa huo ni Liberia, Nigeria na Sierra
Leone na Guinea.
|
No comments:
Post a Comment