MUHIMU/PINGA NDOA ZA UTOTONI SASA:-Watoto 984 waozeshwa kwa nguvu, 1,628 wakeketwa Tarime ..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 27, 2014

MUHIMU/PINGA NDOA ZA UTOTONI SASA:-Watoto 984 waozeshwa kwa nguvu, 1,628 wakeketwa Tarime ..’’

Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo Agosti 27,2014 jijini Dar es Salaam.

Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi.Valerie Nsoka akiwasikiliza.
  
Viongozi mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara, wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.

Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo Agosti 27,2014 jijini Dar es Salaam.

Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.

Baadhi ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.

Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.

Moja ya kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike anavyokabiliana na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike JUMLA ya wasichana wenye umri mdogo wapatao 984 wameolewa na kukatishwa masomo huku wasichana wengine 1,628 wakikeketwa wilayani Tarime, Mkoa wa Mara ikiwa ni miongoni mwa vitendo vya kikatili ambavyo amekuwa akifanyiwa mtoto wa kike baadhi ya maeneo nchini Tanzania.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad