ALAMA ZA MPAKA:- Uzinduzi wa Uimarishwaji wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Burundi leo hii Agosti 27,2014 wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 27, 2014

ALAMA ZA MPAKA:- Uzinduzi wa Uimarishwaji wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Burundi leo hii Agosti 27,2014 wilayani Ngara mkoani Kagera.


Mkazi wa kijiji cha Mugikomero, wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Israel Paul akipaka rangi moja ya alama za mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi ikiwa ni utekelezaji wa programu inayoendelea ya uhuishaji wa mipaka ya kimataifa kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya Kimataifa wa wilaya ya Ngara. (Picha Na:-Maktaba yetu).

Uzinduzi wa Uimarishwaji wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Burundi unafanyika leo hii  Agosti 27,2014 ,Unaofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr.Jakaya Kikwete na Rais wa Burundi  Bw.Piere Nkurunziza.

Uzinduzi huo unafanyika katika kijiji cha Mugikomero,kata ya Mugoma wilayani Ngara mkoani Kagera.



Marais hao pamoja na mambo mengine,Pia watashiriki kujenga jiwe la mpaka kwa kila rais kujenga kwenye upande wa nchi yake, tukio linalotajwa kuwa la Kihistoria.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad