UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
HATIMAYE
kombe la Muliga katika kata ya Kimwani wilayani Muleba mkoani Kagera imefikia
tamani baada ya mzunguko wa ligi ulioshirikisha timu sita za soka
kukamilika na kuchezwa hatua ya fainali ambayo iliahirishwa wiki
mbili zilizopita baada ya kuwepo utata wa kutafuta mshindi wa tatu.
Katika
kuhitimisha ligi ya kombe hilo Timu ya soka ya Viktoria imeibuka mshindi
kwa kuilaza Super Lindanda mabao 4-3 baada ya kulazimika kuitoa kwa
matuta kwani katika dakika 90 timu hizo zilitoka kwa bao 1-1.
Akihitimisha
michuano hiyo mfadhili wa kombe hilo diwani wa kata ya Kimwani Faustini Muliga
alisema alianzisha ligi hiyo si kwa nia ya ushawishi wa kisiasa bali alilenga
kukutanisha vijana na wananchi kwa ujumla ili kuwapa burudani .
Kwenye
mashindano hayo wananchi wa kata hiyo na vijiji vya kata jirani
walihudhuria mpambano wa fainali kupata burudani iliyokuwa na timu shindani
zenye utani wa jadi kati ya Victoria fc na Super Lindanda.
Mjumbe
wa kamati ya ligi hiyo Denisius Didas alitangaza zawadi mbali mbali
na diwani kukabidhi zawadi hizo na kuwataka vijana kuwa na umoja ili kwa
mwakani kuwepo ligi nyingine itakayowakutanisha na wenzao wa kata ya
Nyakabango .
Mshindi wa
kwanza amepata Sh.200 000 na kombe lenye thamani ya Sh 180 000, mshindi wa pili
Sh 150,000 na seti ya jezi pia mshindi wa tatu Vijana fc wamepata
Sh.100 000 huku timu yenye nidhamu KabasharoFc ikipata Sh.20 000.
Hata hivyo
mchezo huo ililalamikiwa na makocha wa timu zote kwa kumuandama mwamuzi katika
mchezo huo aliyesababisha vurugu kuwepo huku jeshi la polisi wakisusia kwa aiina
yake kuimarisha usalama wakati wa upigaji matuta.
No comments:
Post a Comment