IMANI NJEMA:-...Endelezeni yale Mema baada ya Mfungo wa Ramadhani......'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 02, 2014

IMANI NJEMA:-...Endelezeni yale Mema baada ya Mfungo wa Ramadhani......''


Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika msikiti wa Al Nuuru ulioko mjini Muleba  Mkoani Kagera ambapo wametakiwa kuendeleza ibada baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kufanya matendo mema hasa kusaidia yatima na maskini ili kujikinga na adhabu za Mwenyezi Mungu.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

Kaimu Imamu wa msikiti wa Al Nuuru ulioko mjini Muleba  Mkoani Kagera  Idd  Hamdani wakati akitoa salamu za ibada ya sala ya idd na kuwaasa waislamu kumrejea Mungu ili saumu zao ziweze kukubalika. 

Hamdani amesema miongoni mwa sifa za mcha Mungu ni kujihadhari na ulevi wa pombe sigara na madawa ya kulevya na kutumia mali  aliyo nayo muumini kusaidia wasiojiweza na kujiandalia maisha ya mbinguni.

“Waumini walio wengi wanafurahia kuisha kwa ramadhani na kuingia katika anasa kwani hao mungu wo hupatikana mweziramadhani tuu ama siku ya idd pekee hakli hiyo ni kujiandalia makazi mabaya kwa Allah”lisema Idd Hamdani.

Amesema wakati wa mfungo wa Ramadhani waumini walijihadhari na ulevi uasherati utumiaji wa sigara na kutoa misaada mbalimbali lani wema huo wasipouendeleza wataangamizwa siku ya kiama mbele ya mwenyezi Mungu.



Naye Mjumbe wa baraza la maulamaa wilayanmi Muleba  Muhaji  Bushako amewasihi waumini kuzingatia mafundisho ya vitabu vya dini kuhakikisha wanaopewa misaada ni maskini na yatima kwa kuwapati  chakula na vinywaji.

Aidha amewashauri waumini kukutana na kufanya tafakari ya mfungo mtukufu wa Ramadhani ili kubaini walikokwama na kujisafisha kwa kuongeza siku sita za funga  ambazo kwa mujibu wa hadithi za mtume Mohamadi SAW alizisistiza.

Waumini wa kiislamu wa walio wengi Tanzania  wameadhimisha sherehe za sikukuu ya Eid el fitr kwa kukaribishana kwa chakula na vinywaji huku baadhi yao wakiiwaombea dua wazazi , walezi na ndugu zao waliofariki dunia.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad