MAFANIKIO:-Tazama Picha 7 wakati Atletico Madrid ikiifunga bao 1-0 Real Madrid na Kubeba ndoo ya SUPER CUP HISPANIA-Agosti 22,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 23, 2014

MAFANIKIO:-Tazama Picha 7 wakati Atletico Madrid ikiifunga bao 1-0 Real Madrid na Kubeba ndoo ya SUPER CUP HISPANIA-Agosti 22,2014.

Kikosi cha Atletico kikisherehekea na taji la Super Cup jana Agosti 22,2014.

 Real Madrid imeshindwa kuonyesha kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid hapo jana Agosti 22,2014.

Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou.

Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo katika dakika ya 2 tu.

Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza kupindua matokeo.

Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.
Mshambuliaji wa Atletico, Mario Mandzukic akiinua taji la Super Cup baada ya kuifunga Real Madrid jana Agosti 22,2014.




LIGI KUU HISPANIA 2014/2015-LA LIGA-RATIBA

Mechi za Ufunguzi

**Saa za Bongo

Jumamosi Agosti 23,2014.

20:00 Malaga CF v Athletic de Bilbao

22:00 Sevilla FC v Valencia

22:00 Granada CF v Deportivo La Coruna

2359 UD Almeria v RCD Espanyol

Jumapili Agosti 24,2014.

20:00 SD Eibar v Real Sociedad

22:00 FC Barcelona v Elche CF

22:00 Celta de Vigo v Getafe CF

23:59 Levante v Villarreal CF

Jumatatu Agosti 25,2014.

21:00 Real Madrid CF v Cordoba

23:00 Rayo Vallecano v Atletico de Madrid

Ijumaa Agosti 29,2014.

21:00 Getafe CF v UD Almeria

23:00 Valencia v Malaga CF
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad