Profesa Muhongo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Wakizindua Mawe ya Dhahabu na Kuyaonyesha mbele ya waandishi wa Habari ambao
hawapo pichani.
Akitoa
taarifa ya mgodi huo kwa Waziri Muhongo Meneja Mkuu Bw. Denice Sebugwao alisema
STAMIGOLD ilianza uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu tarehe 15/07/2014 katika
Kanda ya Magharibi na tayari mawe mawili ya dhahabu yamezalishwa yenye jumla ya
kilo 25.
Profesa Muhongo akizindua uzalishaji wa tofali la
kwanza la dhahabu alisema kuwa Kampuni ya STAMIGOLD ni Kampuni ya kwanza ya Watanzania kuzalisha
dhahabu nchini, alisema tangu amalize chuo kikuu mwaka 1979 hajawahi kuona
kampuni ya watanzania ikizalisha dhahabu.
Pia waziri
huyo wa Nishati na Madini aliipongeza Kampuni ya STAMIGOLD kwa kuajili kampuni
nyingine za Watanzania ili kukuza upeo mpana wa ajira.
Kampuni zinazofanyakazi
na STAMIGOLD ni SUMA JKT katika ulinzi na Kampuni nyingine ya kuchimba dhahabu
inayoundwa na Wataalamu wa Kitanzania.
Profesa
Muhongo alitoa angalizo kwa Kampuni ya STAMIGOLD kuwa wachape kazi kwa nguvu siku zote kama walivyoanza na isifike
mahali wakazembea na kupelekea kuiua kampuni hiyo.
Pia aliwahakikishia wafanyakazi kuwa wizara ya
Nishati na Madini itahakikisha kampuni hiyo inasimama daima.
|
No comments:
Post a Comment