MAENDELEO:-Hii ni Burudani ya Mwiyeleko ambayo ni Ngoma ya Asili ya Kabila la Wahangaza wilayani Ngara ilivyopendezesha wakati wa Uwekaji Jiwe la Ujenzi wa Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Baramba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 14, 2014

MAENDELEO:-Hii ni Burudani ya Mwiyeleko ambayo ni Ngoma ya Asili ya Kabila la Wahangaza wilayani Ngara ilivyopendezesha wakati wa Uwekaji Jiwe la Ujenzi wa Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Baramba.

Mr  Stefan Tiefethaler kutoka  Nchini Ujerumani (mwenye shati jekundu ) akikata utepe wakati akikagua jengo la bweni la wasichana wa Sekondari ya Baramba iliyoko wilayani Ngara mkoani Kagera August 14, 2014 ambaye ni mmoja wawajumbe wa Shirika la  Marafiki wa Elimu Afrika la Ujeruman ambao ni Wanaofadhili wa shule hiyo, katikati ni  Mr Ernest Wander akishiriki kukata utepe huo akiambatana na Mrs Silvia Fischer.Picha Na:-Shaaban Ndyamukama-Ngara.


Picha juu na chini ni Sehemu ya Burudani ambapo Wajumbe na Wadau wa Elimu kutoka Tanzania na Ujerumani walishiriki kucheza ngoma ya Asili katika Viwanja vya Shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana ya Baramba leo Agosti 14,2014.



Ni kikundi cha ngoma ya Asili cha  baadhi ya Wanafunzi wakitoa  Burudani kwa Wajumbe na Wadau wa Elimu kutoka Tanzania na Ujerumani walishiriki kuweka Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bweni , katika Viwanja vya Shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana ya Baramba leo Agosti 14,2014.

Hiki ni Kikundi cha Ngoma ya Asili kutoka Kumunazi...kikiburudisha kwa kuimba nyimbo za Kabila la Kihangaza.....

Ni Kikundi cha Mwiyeleko ambayo ni ngoma ya Asili kutoka Kijiji cha Mwivuza-Ngara...kikiburudisha kwa kuimba nyimbo za Kabila la Kihangaza wakatika Halfa ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari ya Baramba leo Agosti 14,2014.


Katika uwekaji wa Jiwe la Msingi,Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge mstaafu  wa jimbo la Ngara ,Bw.Gwassa Sebabili (nyuma ya watoto katika picha) ameishauri Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera  kujenga shule za bweni za wasichana wilayani humo ili kunusuru maisha ya wanafunzi wa kike wanaosomea shule za kutwa   na kushindwa kumaliza masomo yao...Kushoto kabisa ni Meneja wa Shule hiyo ya Baramba,Fr.Isias Bambara katika picha ya pamoja nyuma ya jengo hilo.

Mbunge huyo  amesema kuwa  wilaya ya Ngara haina shule ya bweni ya wasichana inayomilikiwa na halmashauri ama serikali na kusababisha wanafunzi wa kike  katika shule za kata kukatiza masomo kwa kukumbana na changamoto mitaani.


Meneja wa shule ya sekondari ya Baramba ,Bw Isias Bambara amesema ujenzi wa bweni la wasichana hadi kukamilika utagharimu Sh 37 mil ambapo 80% ni msaada kutoka marafiki wa Afrika kutoka nchini Ujerumani  na wazazi wamechangia  20% na ujenzi umeanza April mwaka huu.

“Wanafunzi watakaonufaika na bweni hili ni wasichana 100 kati ya  250 wanaoishi katika mabweni saba kati ya hayo matatu ni yenye majina ya Prof.AnnaTibaijuka, Asha Rose Migiro na Anna Makinda ambao ni wanawake maarufu kiutendaji Tanzania”Alisema Meneja.

 Amesema ushirikiano wa marafiki wa Afrika kutoka Tanzania MAT na marafiki wa Afrika wa german MAG ulianza mwaka 1981 chini ya aliyekuwa Askofu wa jimbo la Rulenge marehemu Christopher Mwoleka alipotembelea ujerumani


Katika tukio hilo, Wadau wa Elimu waliokutana Wamewasihi wasichana wa shule hiyo kuwa na uzalendo wa kutumia fedha za wazazi wao kujiendeleza kitaaluma hatimaye kuwa watumishi wa taasisi za   ndani na nje ya nchi huku wakipata Ujuzi,  Maarifa na Maadili kisha  kuwa raia wema,huku  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara ,Bw.John Shim’Imana ametoa wito kwa bodi ya shule ya sekondari  Baramba kushirikiana na halmashauri ya wilaya na wafadhili wa shule hiyo kutafuta wawekezaji ili kupanua urafiki huo na kuboresha mazingira hasa sekta ya utalii.
 
Hata hivyo kiongozi wa wafadhili  wa shule hiyo kutoka nchini Ujerumani Stefan Tiefethaler amesema ushirikiano huo wa marafiki wa afrika na ujerumani hauna budi kuendelezwa kwa kukutana kila mwaka na kutathmini maendeleo na changamoto katika  kuendeleza jamii kielimu

MR. Stefan akikoroga zege pamoja na wadau wenzake kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika bweni la Wasichana wa Shule ya Sekondari ya Baramba ya wilayani Ngara,mkoani Kagera.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad