LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Manchester United yasuasua baada ya kuambulia sare dhidi ya Sunderland-Kesho Agosti 25,2014 ni Man City v Liverpool. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 24, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Manchester United yasuasua baada ya kuambulia sare dhidi ya Sunderland-Kesho Agosti 25,2014 ni Man City v Liverpool.


Unaweza sema Himaya ya Kocha  Louis van Gaal kwenye Ligi Kuu Uingereza 2014/2015  inaendelea kwa kuchechemea baada ya Leo Agosti 24,2014,akiwa ugenini huko Stadium of Light kutoka Sare ya Bao 1-1 na Sunderland na hii ni Mechi yao ya pili ya Ligi baada kuchapwa 2-1 Wikiendi iliyopita na Swansea City

Wakikabiliwa na Majeruhi wengi na pia kushindwa kumchezesha Mchezaji wao mpya Beki Marcos Rojo kutokana na kuchelewa kupata Kibali cha Kazi cha Nchini Uingereza, Man United hii Leo walianza vizuri kwa kufunga Bao katika Dakika ya 17 kupitia Juan Mata baada ya pasi ya Antonio Valencia.


Sunderland walisawazisha katika Dakika ya 30 kutokana na Kona ya Seb Larsson na kumkuta Jack Rodwell akiwa pekee aliemalizia kwa kichwa.


Man United walipata pigo kabla ya Haftaimu baada ya Chris Smalling kuumia na ikabidi Chipukizi wa Miaka 21, Michael Keane, kuingia kucheza Mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi akisaidiana kwenye Difensi ya Mtu 3 ya Chipukizi Tyler Blackett na Phil Jones.

Kipindi cha Pili Man United mara mbili walilalamikia kunyimwa Penati na Refa Martin Atkinson, ambae tangu enzi za Sir Alex Ferguson amekuwa hana rekodi nzuri nao, na Refa huyo kukataa kutoa na kudiriki hata kumpa Kadi ya Njano Ashley Young kwa kumtuhumu amejiangusha.

Kabla ya Mechi ijayo ya Ligi kwa Man United Jumamosi ijayo ambayo watacheza Ugenini na Timu iliyopanda Daraja Burnley, Jumanne Usiku watakuwa Ugenini kucheza na MK Dons kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Capital One Cup.


Jumatatu Agosti 25,2014.

2200 Man City v Liverpool

Jumamosi Agosti 30,2014.

1445 Burnley v Man United

1700 Man City v Stoke

1700 Newcastle v Crystal Palace

1700 QPR v Sunderland

1700 Swansea v West Brom

1700 West Ham v Southampton

1930 Everton v Chelsea
Jumapili Agosti 31,2014.

1530 Aston Villa v Hull

1800 Leicester v Arsenal


Mshambuliaji wa Spurs, Emmanuel Adebayor akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR Uwanja wa White Hart Lane. 

Tottenham walianza vyema Mechi hii ya leo Agosti 24,2014 ya Nyumbani White Hart Lane na hadi Mapumziko walikuwa mbele kwa Bao 3-0 zilizofungwa na Nacer Chadli, Bao 2 za Dakika za 12 na 37, na moja la Eric Dier katika Dakika ya 30.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 65, pasi ya Danny Rose ilimaliziwa vizuri na Emmanuel Adebayor aliefunga Bao la 4 kwa Tottenham.

Hadi mwisho Spurs 4 QPR 0 na huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Tottenham tangu Ligi ianze Wiki iliyopita Agosti 16,2014.

As It Stands Table


Position Team Played Goal Difference Points
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Moving up 1 Tottenham 2 5 6
Moving down 2 Chelsea 2 4 6
Moving down 3 Swansea 2 2 6
Moving down 4 Arsenal 2 1 4
Moving up 5 Hull 2 1 4
Moving down 6 Aston Villa 2 1 4
Moving down 7 Man City 1 2 3
Moving down 8 West Ham 2 1 3
Moving down 9 Liverpool 1 1 3
No Movement 10 Everton 2 0 2
Moving up 11 Sunderland 2 0 2
Moving down 12 West Brom 2 0 2
Moving up 13 Man Utd 2 -1 1
Moving down 14 Southampton 2 -1 1
Moving up 15 Stoke 2 -1 1
Moving down 16 Leicester 2 -2 1
Moving down 17 Newcastle 2 -2 1
Moving up 18 Crystal Palace 2 -3 0
Moving up 19 Burnley 2 -3 0
Moving down 20 QPR 2 -5 0


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad