TEKNOLOJIA:-Soma Jinsi Kompyuta na Simu zinavyomaliza Nguvu za Kiume na Kusababisha Ulemavu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 31, 2014

TEKNOLOJIA:-Soma Jinsi Kompyuta na Simu zinavyomaliza Nguvu za Kiume na Kusababisha Ulemavu.


Watanzania wametakiwa kuwa makini wanapotumia simu na kompyuta, kwani ndio chanzo cha matatizo mbalimbali yakiwemo ya kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.

Mshauri wa masuala ya teknolojia, Alex Mpompo aliyasema hayo Julai 29,2014 kwenye semina inayohusu teknolojia katika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Mpompo alisema matatizo yanayochangiwa na teknolojia yapo mengi ikiwamo kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.

Alisema vijana wengi nchini wana upungufu wa nguvu za kiume jambo linalochangiwa na matumizi mabaya ya teknolojia hivyo kuchangia familia kusambaratika.

Aliwaasa Watanzania kutotumia kompyuta kwa muda mrefu kwa kuipakata kwenye mapaja, kwani mionzi inapenya kwa urahisi katika maeneo hayo na kuathiri mbegu za kiume na kusababisha ugumba.

Watu wengi hawaelewi kama ukiweka simu karibu na jiko la gesi unaweza kuunguza nyumba, pia unapogandamiza simu na ngozi inasababisha saratani ya matiti na ugonjwa wa moyo..alisema Mpompo.

Alisema vijana wanaoongea na simu kwa muda mrefu wapo kwenye hatari zaidi ya kupoteza kumbukumbu na kutosikia.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.

Like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad