AJALI YA BASI DODOMA:- Dedeva alikuwa anaonyesha Mwanafunzi hawezi Kumpita..’’huku Watu waliokufa katika ajali hiyo ya Basi la MORO BEST imeongezeka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 31, 2014

AJALI YA BASI DODOMA:- Dedeva alikuwa anaonyesha Mwanafunzi hawezi Kumpita..’’huku Watu waliokufa katika ajali hiyo ya Basi la MORO BEST imeongezeka.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime amesema tukio hilo la Pandambili Wilayani Kongwa katika barabara ya Dodoma – Morogoro julai 30,2014,Asubuhi limesababisha vifo vya watu 18 wanaume watu wazima 11 na mtoto mmoja wa kiume na Wanawake watu wazima 5 na mtoto 1 wa kike.
Majina ya Marehemu hao ambao wametambuliwa na ndugu zao na kusafirishwa kwenda makwao kwa maziko ni:-

 1.   Christina d/o Dickson, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Mpwapwa

 2.   Omari s/o Mkubwa, Miaka 32, Muhaya, Kondakta wa bus, Mkazi wa Morogoro

 3.   Malick s/o Masawe, Miaka 42, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mpwapwa

 4.   Wilson s/o Paul @ Suda, Miaka 63, Mgogo, Mstaafu  Red Cross, Mkazi wa Mpwapwa.

 5.   Said s/o Lusogo, Miaka 44, mluguru, dereva wa bus, Mkazi wa Kihonda Morogoro.

 6.   Gabriel s/o Meja @ Chiwipe, Miaka 50, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa

 7.   Gilbert s/o Lemanya, Miaka 53, Mgogo, dereva wa Lori, Mkazi wa Makole Dodoma

 8.   Mikidadi s/o Zuberi @ Omari Miaka 22, Mbondei, Tingo wa Lori, Mkazi wa Morogoro/Ilala Dar es Salaam.

9.   Justine s/o Makasi, Miaka 24, Mgogo, Mkulima wa Mpwapwa

10.       Alice d/o Masingisa, Miaka 24, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa

11.       Merina d/o Doto @ Marcel, Mgogo, Miaka wa Mji mpya  Mpwapwa

12.       Nasibu s/oSeif, Miaka 48, Mkazi wa Morogoro

13.       Nicholaus s/o Raymond Kileo Miaka 51, Mkazi wa Mpwapwa

14.       Stella d/o Mdako, Miaka 60, Mkazi wa Mpwapwa

15.       Erick s/o Lucas,Miaka 10, Mkazi wa Morogoro

16.       Nazaret s/o Deremsi @ Kasuga, Miaka 45, Mhehe,  Mfanyabiashara, Mkazi wa     Kibakwe Mpwapwa.

17.       Darini d/o Dickson, Miaka 2, Mgogo, Mkazi wa Mpwapwa

18.       Magreth d/o Nyanzi, Miaka 35, Mgogo, Mfanyabiashara, Mkazi    wa Mwananyamala Dar es Salaam.

Aidha majeruhi waliokuwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa wametibiwa na kuruhusiwa na wengine kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.
 
Waliobaki katika Hospitali ya Mkoa wakiendelea na matibabu ni 32 na wanaendelea vizuri isipokuwa walio katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu wa madaktari (ICU)  ambao ni George s/o Mjelwa, Miaka 40, Daktari wa Wilaya ya Mpwapwa na mke wake aitwaye Getrudar s/o Kombe, Miaka 37, Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

Jana kamanda alisema ajali hiyo baada ya uchunguzi zaidi inaonyesha kusababishwa na madereva wote wawili kwa maana ya dereva aliyekuwa anaendesha lori namba T 820 CKU/T390 CKT GILBERT S/O LEMANYA kwa kupita gari lingine bila kuwa mwangalifu na magari yaliyokuwa yanatokea mbele yake na kuwa katika mwendo kasi.

Dereva wa bus namba T 858 AUH SAID S/O LUSOGO kulingana na mashuhuda hasa abiria wanaeleza alikuwa mwendo kasi na ndiyo maana ajali hii imeleta madhara makubwa kiasi hicho kwani kama angelikuwa kwenye mwendo wa kawaida unaotakiwa madhara yangekuwa siyo makubwa kiasi hicho pamoja na dereva wa lori kufanya aliyofanya.

Wito kwa madereva na watumia barabara wengine waache mwendo kasi na ushabiki wa ushindani kwani kulingana na ushahidi uliokusanywa unaonyesha dereva wa Moro best alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi kutaka kwenda kulipita bus la AL-SAEDY lililokuwa limeondoka mbele yake kwa kigezo kuwa dereva wa bus hilo ni mwanafunzi wake hivyo hawezi kufika Morogoro kabla yake.

Wamiliki wa Ma bus na magari mengine wawaonye madereva wao kuhusiana na mwendo kasi na kuwataka wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali mbaya kama hii.

Aidha abiria wasiwe wanakaa kimya kama walivyofanya wa bus la Moro best wanapoona dereva anaendesha kwa mwendao wa kasi watoe taarifa Polisi ili wakamatwe na kuepusha madhara kama yaliyotokea. 

Imetolewa na:-
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.

Like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad