Katika Baraza hilo la Eid el Fitir lilofanyika Eid pili,Julai 30,2014- Kiasi cha shilingi milioni 2 laki 7 na elfu 93
zimechangwa na waumini wa madhehebu ya
dini wakiwemo viongozi wa chama na serikali wilayani Ngara mkoani Kagera kwa
ajili ya ujenzi wa msikiti wa Mugoma
wilayani Ngara.
Picha zote Na:-Shaaban Ndyamukama.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Baraza kuu la Waislamu (BAKWATA
)Wilayani Ngara Bw Michael Ndyamukama amesema kati ya fedha hizo ambazo ni taslimu, Shilingi laki 3 na elfu 14
ni ahadi ni Shilingi milioni 2 laki 4 na elfu 80.
Bw Ndyamukama amesema fedha hizo zimepatikana jana wakati wa baraza
la idd katika harambee iliyofanyika kata
ya Mugomwa na malengo ni kukamilisha
ujenzi wa msikiti huo ili waumini wapate sehemu ya kufanyia ibada kwa pamoja.
Hata hivyo amewataka waumini kuhakikisha wanawapatia
watoto wao elimu ya maadili kupitia shule za dini na elimu ya kukabiliana na
changamoto za maisha kupitia mfumo wa elimu ya msingi na sekondari kuwawezesha kuwa raia wema.
|
No comments:
Post a Comment