Mchezo huo
ambao ulikuwa na kila aina ya ufundi kutoka kwa wachezaji wa timu zote kipindi
cha kwanza kilimalizika baada ya timu hizo kutosha nguvu ya 0-0
Katika kipindi
cha Pili timu hiyo inayoongozwa na Kocha Mchezaji Aman Richard ilifanya
mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ambapo katika safu ya ushambuliaji aliingia
Augustine Mgendi mabadiliko ambayo yaliinufaisha timu hiyo ya Biashara United
baada ya mchezaji huyo kuifungia timu hiyo mabao hayo mawili.
Akiongea
baada ya mchezo huo,Kocha huyo alisema kuwa bado timu hiyo inahitaji kufanya
maboresho kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge Mjini Dodoma.
“Tumeshinda
mchezo wetu lakini bado tuna kazi kubwa maana tunapata nafasi nyingi lakini
hatuzitumii ipasavyo,sasa kwa mchezo uliopo mbele yetu lazima tubadilike”
alisema Kocha Aman.
Katika
mchezo huo ambao ulishuhudiwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara, ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge utakaofanyika
mwanzoni mwa mwezi August,mwaka huu mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment