Wachezaji wa
Timu ya Taifa ya Cameroon wakichapana katika mechi yao uwanjani wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2014.
|
Shirikisho
la soka Ulimwenguni FIFA linataka uchunguzi uwe wazi juu ya Tuhuma hizo.
|
Maafisa wa
Cameroon watapelelezwa kutokana na madai saba ,kwamba kati ya wachezaji wa timu
ya taifa hilo walihusika katika kupanga mechi katika Kombe la Dunia
2014,linaloendelea nchini Brazil.
Kamati ya
maadili ya shirikisho la kandanda la taifa hilo litachunguza shutuma za
"udanganyifu" wa "wachezaji saba wabaya" katika mechi zao
tatu za makundi.
Madai hayo
yametolewa na gazeti moja la kijerumani na mtu aliyehukumiwa kwa kuhusika na
kupanga mechi nchini Singapore.
Cameroon
ilipoteza mechi zote za kundi A, ikiwemo ile waliolazwa na Croatia kwa mabao
4-0.
Mchezaji wa
'The Indomitable Lions' Alex Song, alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumgota Mario
Mandzukic mgongoni katika mechi hiyo, huku wachezaji wenzake Benoit
Assou-Ekotto na Benjamin Moukandjo wakizozana baadaye katika mechi hiyo.
Ripoti
kutoka katika shirikisho la kandanda la Cameroon lilisema: "Madai yaliyotolewa
majuzi kuhusu udanganyifu katika mechi tatu za mwanzo za Cameroon katika Kombe
la Dunia la 2014, hasa kati ya Cameroon na Croatia, na vile vile 'kuwepo na
wacheza saba wabaya katika timu yetu ya taifa' hayaambatani na maadili na
kanuni zinazopendekezwa na usimamizi wetu, pamoja na kanuni za Fifa na maadili
ya taifa letu.
"Tuna
nia kuu ya kutumia mbinu zote zinazostahili ili kutatua swala hili linalosumbua
kwa muda mfupi iwezekanavyo."
'FIFA yataka
uchunguzi wa wazi'
Fifa
haikusema iwapo ilikuwa ikichunguza swala hilo au la, kwani bodi hiyo
inayosimamia kandanda ulimwenguni "ilitaka uchunguzi uwe wazi".
Hata hivyo,
iliongezea kuwa: "kwa ujumla, uadilifu katika mchezo huu ndio swala
linalopewa kipaumbele na Fifa, kwa hivyo, tunatilia madai yoyote kuhusu
udanganyifu maanani sana."
'Mgogoro wa
marupurupu'
Matayarisho
ya Cameroon kabla ya michezo hiyo nchini Brazil yalitatizika baada ya wachezaji
kukataa kupanda ndege kuelekea Brazil hadi wakati mgogoro uliohusiana na
wachezaji hao kulipwa marupurupu yao ulipotatuliwa.
Maelewano ya
fedha hatimaye yalifikiwa na shirikisho la kandanda la Cameroon, Fecafoot,
lakini safari ya kikosi hicho kuelekea Brazil ilikuwa imecheleweshwa kwa
takriban siku nzima.
Walianza
michezo hiyo kwa kushindwa kwa bao 1-0 na Mexico kabla ya kulazwa na Croatia na
wenyeji Brazil waliowafunga mabao 4-1.
"Wachezaji
kadhaa walikosa nidhamu, na ndio sababu tumefungwa mabao manne," mkufunzi
wa Cameroon Volker Finke aliambia gazeti la kifaransa la L'Equipe baada ya
kushindwa na Croatia.
"Ninajua
ni vigumu kucheza na wachezaji kumi, lakini hilo si sababu ya kupoteza katika
mkondo huu.
"Mechi
ilikuwa sawa hadi tulipoonyeshwa kadi nyekundu. Wacroatia walifanya vizuri
mbele ya lango lakini Cameroon pia ilikuwa na nafasi ya kufunga.
"Tabia
ya wachezaji kadhaa kwa kweli sio nzuri. Hata tulipokuwa bado na wachezaji 11
kila upande, haikuwa ya kupendeza.",(A.I)
No comments:
Post a Comment