Muonekano wa Vikapu vilivyotengenezwa kwa mikono kwa kutumia malighafi za kiasili na Wajasirimali wa
wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera .
|
Mkuu wa
wilaya ya Biharamulo
Mkoani Kagera,Bw.
Richard Mbeho.
|
Mkuu wa
wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera Bw Richard Mbeho amepiga marufuku tabia ya
wakazi wa wilaya hiyo kunywa pombe nyakati za asubuhi, badala yake watumie muda
huo kufanya kazi ili kuchochea Maendeleo.
Akihutubia
katika Mkutano wa Sherehe za Serikali za Mitaa zilizfanyika kiwilaya katika
kijiji cha Katoke, Kata ya Nyarubungo, Bw Mbeho amesema unyaji wa pombe umekuwa
kikwazo cha Maendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kunywa pombe saa za kazi.
Amesema ni
wajibu wa kila mwananchi kutumia muda wa Kazi kufanya shughuli za maendeleo
badala ya kuanza kunyw apombe kuanzia asubuhi hadi jioni na wakati mwingine
usiku wa manane ambapo amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwashughulikia
watu wa aina hiyo.
Katika Hatua
nyingine Bw Mbeho amewataka Watumishi wa umma kuzingatia maadili huku Wenyeviti
na Watendaji vijiji na kata wakitakiwa kuitisha mikutano na kuwasomea wananchi taarifa
za mapato na matumizi.
Pia
amewataka wakazi wa wilaya hiyo
kuhakikisha wanatunza akiba ya mazao ya nafaka na kuepuka kuyatumia
kutengenezea Pombe ili kuepukana na Baa la njaa wilayani humo.
No comments:
Post a Comment