Mwili wa Mawazo Wilbard Kazungu (31) ukiwa nyumbani kwake ukining'inia
baada ya kujinyonga katika chumba cha kulala
watoto wake .
|
Eneo la chumba ambako alikaa
kitandani na kunywa dawa ya kuoshea mifugo kisha kupanda stuli na kujitundika
kamba
|
Vijana walio kuwa na ukaribu na
marehemu wakiwemo ndugu zake wakiubeba mwili wa marehemu kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi chini ya jeshi la polisi
|
Mganga mfawidhi wa kituocha Afya
Mabawe Juvent John akifanya uchunguzi wa mwili wa marehemu Mawazo baada ya
kuuondoka kwenye kamba
|
Wananchi wakiwa mbele ya nyumba ya
marehemu Mawazo katika kushuhudia mwili ukiondolewa kwenye kamba kwenye chumba
alikojinyongea
|
Wananchi wakiwa katika tukio la
Mwazo Kazungu aliyejinyonga wakitafakari matukio ya kujinyonga wilayani Ngara
|
Wananchi wakiwa katika nje ya nyumba ya Marehemu
Mawazo Kazungu wakizungumzia maisha yake wakati wa uhai wake kabla hajajinyonga
|
NGARA
Kijana mmoja
mkazi wa kijiji cha Mukaliza wilayani Ngara mkoani Kagera aliyetambulika kwa
jina la Mawazo Wilbard Kazungu (31) jana Juni 2014 amekutwa amejinyonga
nyumbani kwake katika chumba cha kulala watoto wake
Afisa
mtendaji wa kijiji cha mukaliza Joseph Festo amesema kijana huyo alijinyonga
kwa kutumia kamba ya kufungia mifugo aina ya katani na kabla ya kujitia kitanzi
alianza kunywa dawa ya kuoshea ng'ombe na ndipo aliingiza shingo katika fundo
la kamba ikitokea katika paa la nyumba yake.
Festo
alisema tukio hilo lilitokea saa 6 mchana ambapo mke wake alikuwa amekwenda
shambani na aliporejea alimkuta mumewe akining'inia chumbani akiwa tayari
ameshafariki huku chini ya kitanda cha watoto wao kukiwa na kopo la dawa ya
ng'ombe ambalo alilifungua na kunywa dawa hiyo.
Alidai kuwa
katika maisha ya kijana huyo alikuwa ni mjasiliamali wa kuuza mifugo na mazao
mbalimbali katika kata ya mabawe kwa kujiongezea kipato kiuchumi na alikuwa
hajashtakiwa kwa dhuluma bali aliishi vema na wananchi wake pamoja na jamaa
wakiwemo marafiki.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Mukaliza Manase Rutegama amesema kuwa marehemu mawazo wakati wa uhai wake hajawahikuwa na ugomvi wa kifamilia na alikuwa akifanya shughuli bila kuwa na migogoro yoyote.
"Viongozi na wanafamilia tumepokea kifo hicho kwa mshituko na katika kata ya mabawe wananchi walikuwa hawajapata kupata mtu aliyejinyonga na huyo kijana kaacha watoto watatu na mke mmoja".Alisema Rutegama.
Katika kutungua mwili wa marehemu kwenye kamba chini ya jeshi la polisi mganga mfawidhi wa kituo cha afya mabawe Juvent John alisema kamba ndiyo ilikatisha maisha yake baada ya kuziba mishipa ya damu na kukata mawasiliano ya kupumua
Hata hivyo jeshi la polisi licha ya kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho limewataka wananchi kuwa na ulinzi shirikishi kuhakikisha kila mmoja anatambua shda za mwenzake na kutoa taarifa katikavyombo vya dola kwa yule aliye na maoni ya kutaka kujiondoa nafsi yake ama kufanya matukio ambayo ni makosa ya jinai.
mmoja wa askari polisi jamii aliyetambulika kwa jina la Oscar alisema katika jeshi la plisi kuna dawati la ushauri nasaha kwani matukio ya kujinyonga wilayani Ngara yanazidi kuongezeka hasa kwa kuhusisha kundi la vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Alisema wanaobaki wakiteseka kutokana na matukio hayo ni akina mama na watoto na wazee waliokuwa wategemezi wa vijana hao na wananchi kwa imani zao hawana budi kusali pamoja kuomba Mungu kuepusha jinamizi hilo la watu kujinyonga.
Habari/Picha Na:-Shaaban Ndyamukama-Ngara.
No comments:
Post a Comment