AFCON 2015 DHIDI YA MSUMBIJI:-Taifa Stars yatunguliwa 4-2 na Botswana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 01, 2014

AFCON 2015 DHIDI YA MSUMBIJI:-Taifa Stars yatunguliwa 4-2 na Botswana.


Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 4-2 na wenyeji, Botswana leo Julai 01,2014, mjini Gaborone katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki. 

 Mabao ya Stars yalifungwa na Khamis Mcha 'Vialli' na John Bocco 'Adebayor' kwa penalti. 


Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad