|
Jina la Tanzania linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika
maandamano ya ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe kabambe
za ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow, Scotland, uliobeba
watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia live sherehe hizo kupitia
katika TV zao.
Takriban mashabiki 100,000, na wanamichezo 4,000
kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana wapo hapo kwa michezo hiyo ambapo hii ni
mara ya 20 kufanyika toka ianzishwe.
|
|
Sehemu ya wanamichezo wa Tanzania kwenye sherehe hizo za ufunguzi. Jumla
ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada
za Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa
Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao
wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand.
|
|
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Suleiman Mjaya Nyambui (T-shirt ya
njano) akihamasisha vijana wake ambapo Mbali na judo, mpira wa meza, ndondi na
kuogelea, Tanzania pia inawakilishwa na timu za baiskeli na riadha.
|
|
Nahodha na bondia wa Tanzania Seleman Salum Kidunda akipeperusha juu
bendera ya Taifa wakati akiongoza wenzake kwenye maandamano hayo ya ufunguzi
Julai 23,2014 na Michezo hiyo ya 20 ya Jumuiya ya Madola inatarajiwa kudumu kwa
siku 11 katika michezo 17 tofauti.
|
|
...........Nembo ya mashindano ya Jumuiya ya madola.................
|
Mashindano
ya Jumuiya ya Madola yameanza leo Julai 24,2014, mjini Glascow Scotland na kufunguliwa rasmi na
Malkia Elizabeth wa Uingereza ambaye pia ni mkuu wa nchi wanachama wa Jumuiya
ya madola.
Zaidi ya
wanariadha elfu tatu wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayodumu
kwa muda wa majuma matatu yajayo.
Australia
ndio nchi ambayo imetuma kikosi kubwa zaidi katika mashindano haya ya mwaka
huu.
Takwimu
rasmi zinasema kuwa Australia inaawakilishwa na zaidi ya wanariadha 400.
Mataifa yote
nchi wanachama wa muungano huo kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kati
yamewakilishwa kwenye mashindano ya mwaka huu.
Ushindani
mkali unatarajiwa kuonekana katika fani mbali mbali za michezo na macho yote ya dunia
, itakuwa katika shindano la riadha ambalo litatumiwa na mataifa mengi kuchagua
vikosi vyao vitakavyoshiriki katika mashindano ya mabara na hatimaye kombe la
dunia.
Mashindano
haya yataanza rasmi hiyo leo huku wanariadha kadhaa wa Afrika Mashariki
wakijibwaga ugani kuchuana na wapinzani wao katika raundi ya kwanza ya
mashindano ya Judo, Masumbwi na Table tennis.
No comments:
Post a Comment