Mafunzo ya
stashahada ya ualimu wa shule za msingi (Ordinary Diploma in Primary
Education
(ODPE) katika vyuo teule vya majaribio na stashahada maalumu ya Ualimu wa
Sekondari kwa waliomaliza Kidato cha Nne (Hisabati na Sayansi), yataanza
kutolewa katika Chuo Kikuu cha Dodoma na yataanza rasmi Oktoba 6, mwaka huu.
Taarifa ya
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) iliyotolewa jana mjini hapa, ilisema
uombaji wa nafasi za mafunzo hayo kwa mwaka 2014/15 ulianza Juni 23, mwaka huu,
utamalizika Agosti 31, mwaka huu.
Taarifa hiyo
ilisema mafunzo yatatolewa katika vyuo vilivyoteuliwa na Nacte, na baadhi ya
vyuo vitatoa mafunzo hayo chini ya uangalizi wa karibu wa baraza hilo, Taasisi
ya Elimu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Katibu
Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Primus Nkwera alisema waombaji wote wanatakiwa
kuzingatia utaratibu wa uombaji ambao ni kupitia njia ya mtandao ya mfumo wa
udahili wa pamoja (Central Admission System - (CAS) inayopatikana kwenye tovuti
ya CAS au baraza na hawatamtambua mwombaji yeyote atakayeomba kinyume na
utaratibu uliowekwa.
Dk Nkwera
alisema lengo la mafunzo hayo ni kutoa nafasi kwa walimu wa shule za msingi
kuongeza uwezo na kujiendeleza kwa masomo ya ngazi ya juu.
Alisema
katika taarifa yake kuwa kwa muda mrefu walimu wa shule za msingi hawana namna
ya kuongeza na kuboresha taaluma yao kutokana na kutokuwepo kwa kozi ya namna
hiyo.
No comments:
Post a Comment