Madaktari
nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik
Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .
|
Dr Sunanda
Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai
ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik
aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu
makali.
Madaktari
wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai
kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.
Dr Dhiware
anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi
kukutana na tukio la namna hiyo.
Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu
vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno
yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni
kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno
232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida
wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi
wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa
akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni
matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.
Habari Na:-BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment