AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA MH17 :- Tazama Taswira ya Miili ikiwasili Mjini Eindhoven Nchini Uholanzi kwa Taratibu za Maziko. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 24, 2014

AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA MH17 :- Tazama Taswira ya Miili ikiwasili Mjini Eindhoven Nchini Uholanzi kwa Taratibu za Maziko.

Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven ambapo Ndege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.


Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.


Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven Nchini Uholanzi.


Mfalme na Malkia wa Uholanzi , Waziri mkuu na Viongozi wengine  walishiriki huko Eind-hoven pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya Marehemu.


Vifaa vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi . 

Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.

Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.

Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad