Emmanuel
Mbasha (32) akiwa na baba yake mzazi Mahakamani ambapo kesi imeahirishwa hadi August 22,2014. |
KESI ya
ubakaji inayomkabili Mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo
za injili Tanzania, Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23,2014 katika
mahakama ya wilaya ya Ilala ,Jijini Dar es Salaam ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku
akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.
Akisoma hoja
hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, Mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro
Katunga alisema May 23,2014,Mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye Yerusalemu
Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo
wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani.
Katunga
aliendelea kufafanua kuwa May 25,2014, Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji
baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo
nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.
Hizo
sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.
Hata hivyo
iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa katika kituo cha
polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu ambapo
uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti huyo aliingiliwa kimwili.
Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka binti huyo.
Alichokubali
ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye
hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23,2014 mke wake Flora Mbasha
hakuwepo nyumbani.
Baada ya
kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago
aliahirisha kesi hiyo hadi August 22,2014 baada ya wakili anayemtetea Mbasha
kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya Mkoa.
No comments:
Post a Comment