KUTWAA KOMBE LA DUNIA 2014 KUNA RAHA:- Mtazama Mario Gotze akila bata na Demu wake…’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 18, 2014

KUTWAA KOMBE LA DUNIA 2014 KUNA RAHA:- Mtazama Mario Gotze akila bata na Demu wake…’’

 Nyota aliyewapa Ujerumani kombe la dunia 2014,Mario Gotze akila bata na mpenzi wake, mwanamitindo, Ann-Kathrin Brommel.

MARIO Gotze, maisha yanamwendea safi kabisa.

Akitokea kushinda  kombe la dunia na nchi yake ya Ujerumani baada ya kufunga bao la dakika za nyongeza, mshambuliaji huyo wa Bayern Munich ameanza likizo akiwa na demu wake kipenzi,  Ann-Kathrin Brommel maeneo ya Ibiza.

Wawili hao wamepigwa picha wakifurahia maisha kwenye jua tamu  juu ya boti.

Angalau nyota huyo mwenye miaka 22 anastahili kufanya hivyo baada ya kutoa mchango wake wa kuwafanya Ujerumani wawe mabingwa wa dunia nchini Brazil.



Nifunike `hanii`: wawili hao wakila bata baada ya kushinda kombe la dunia majira haya ya kiangazi nchini Brazil.

Anajivunia kidume: Brommel yupo likizo na Gotze baada ya kiungo huyo wa Ujerumani kushinda kombe la dunia.

Brommel alionekana uwanjani nchini Brazil baada ya Ujerumani kutwaa `ndoo` ya dunia .

Gotze akipumzika maeneo ya  Ibiza, Hispania, baada ya kufunga bao zuri lililowapa ubingwa Ujerumani wa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

 Gotze akiwa mapumzikoni kabla ya kurudi kuungana na Bayern Munich katika harakati za msimu mpya wa 2014/2015 wa Bundesliga.

Shangwe: Mshindi wa mechi,  Gotze alisema wachezaji wa Ujerumani wanatakiwa kufurahia pati `bab kubwa` baada ya kushinda kombe la dunia.  


Gotze na Andre Schurrle wakishangilia ubingwa wa Ujerumani mjini Berlin.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad