Mume wa
mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha Jana (Al Hamis Julai 17,2014)
amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala,Jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka
mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi
hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa
muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini
alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo
ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na
wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo imeanza Mbasha
hajapeleka wakili yoyote.
Mara baada
ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha
barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba
kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel
Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa
hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa
mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na
badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii
imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment