KOMBE LA DUNIA 2014:-Yaliyojili wakati Rais Obama na Wamarekani wakitolewa na Ubelgiji kwa bao 2-1 huku Lionel Messi na Di Maria wakiibeba Argentina kwenda Robo Fainali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 02, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Yaliyojili wakati Rais Obama na Wamarekani wakitolewa na Ubelgiji kwa bao 2-1 huku Lionel Messi na Di Maria wakiibeba Argentina kwenda Robo Fainali.

Goli la Dakika ya 118 la Angel Di Maria limewapa Argentina ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Switzerland kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia huko Brazil na kuwaingiza Robo Fainali na watakutana na Ubelgiji waliowatoa Marekani kwa kushinda bao 2-1.

 Licha ya kutawala, Argentina walishindwa kuipenya Switzerland na mchezo
kumalizika 0-0 baada Dakika 90 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Nyota huyo wa Real Madrid aliitendea haki pasi nzuri ya Lionel Messi wa Barcelona dakika ya 118 kuipeleka Argentina Robo Fainali ya Kombe la Dunia.

Tofauti na ilivyotarajiwa akina Messi wangefuzu kiulaini, Uswisi waliibana Argentina na ilibaki kidogo mshindi aamuliwe kwa matuta.   
Mpenzi na Mwanaye Lionel Messi wakiwa Jukwaani kutazama ambapo katika mchezo huo Messi alikimbia na mpira umbali mrefu kabla ya kutoa pasi kwa Angel di Maria aliyeumalizia wavuni dakika ya 118 na kuipa Argentina ushinidi wa bao 1-0 dhidi ya Uswis.
Wamarekani karibu viwanja vyote vya michezo nyumbani kwao vilikuwa vimejaa mashabiki wakishuhudia mechi hiyo huku wakiongozwa na Rais wao Barack Obama.
Timu ya Taifa ya Ubelgiji imeing’oa USA/Marekani katika michuano ya Kombe la Dunia na kusonga hadi hatua ya robo fainali baada ya kuichapa kwa mabao 2-1.

Mechi hiyo ngumu, tamu na yenye upinzani mkali ilimalizika baada ya dakika 120 kutokana na 90  kumalizika ikiwa 0-0 katika mchezo huo uliochezwa huko Estadio Fonte Nova Jijini Salvador.

Hii ni mara ya kwanza katika Miaka 28 kwa Ubelgiji kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia na Jumamosi Julai 05,2014,wataivaa Argentina ambao nao walitumia Dakika 120 kuibwaga Switzerland Bao 1-0 mapema Jana(Julai 01,2014).

Katika Dakika ya Pili tu ya muda wa Nyongeza wa Dakika 30, Kevin de Bruyne alimaliza ubishi wa USA kwa kufunga Bao na Romelu Lukaku, alietokea Benchi, akapiga Bao la Pili Dakika 11 baadae na kuifanya Ubelgiji  iongoze 2-0.

Lakini USA wakapata matumaini baada Julian Green kupiga Shuti lililomshinda Kipa Thibaut Courtois na kufanya iwe 2-1 huku Jermaine Jones na Clint Dempsey kukosa nafasi za kuisawazishia USA.

Bila shaka, USA chini ya Kocha Mjerumani Jurgen Klinsmann, wanapaswa kumshukuru sana Kipa wao Tim Howard ambae aliweka Historia ya kuokoa michomo mingi katika Mechi moja.
Romelu Lukaku wa Ubelgiji kulia akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Ubelgiji bao la pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Marekani mchezo wa mwisho wa 16 Bora Kombe la Dunia nchini Brazil jana Julai 01,2014, usiku huu.  Jumatano ni mapumziko na Robo Fainali zitaanza kuchezwa Ijumaa Julai 04,2014.
KOMBE LA DUNIA
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
**Saa za Bongo.

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil 1-1 Chile , Penati 3-2
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia 2- 0 Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands 2-1 Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica 1-1 Greece, Penati 5-3
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France 2-0 Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany 2 -1 Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina 0-0 Switzerland [Dak 120, 1-0]
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium 0 -0 USA  [Dak 120, 2-1]
Fonte Nova
Salvador







ROBO FAINALI-IJUMAA, JULAI 4, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
France v Germany [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

2300
Brazil v Colombia [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza

JUMAMOSI, JULAI 5, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Argentina v Belgium [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia

2300
Netherlands v Costa Rica [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador


NUSU FAINALI-JUMANNE, JULAI 8, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte

JUMATANO, JULAI 9, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 59 Mshindi 60 [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo


MSHINDI WA TATU-JUMAMOSI, JULAI 12, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia


FAINALI-JUMAPILI, JULAI 13, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad