EID MUBARAKA..! Taswira ya Waislamu walivyoswali Sala ya Eid el Fitir viwanja vya Kokoto Mjini Ngara-Julai 29,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 29, 2014

EID MUBARAKA..! Taswira ya Waislamu walivyoswali Sala ya Eid el Fitir viwanja vya Kokoto Mjini Ngara-Julai 29,2014.


Ni shamrashamra za kusherehekea siku takatifu ya Eid el Fitiri Mjini Ngara ambapo Waumini wa Kiislamu walikusanyika kwa Sala katika Viwanja vya Kokoto ikiwa ni tukio jema  baada ya kumaliza Swaumu ya siku 30 ya Mwezi wa Ramadhani Julai 29,2014.


Kipindi hiki kilikuwa ni cha kujizuia kula na kunywa nyakati za mchana hadi muda wa magharibi (jioni) kwa kufuturu chochote.

Katika kipindi hicho waumini hao walikuwa wakijizuia katika kutenda maovu pia na kujikithirisha zaidi kufanya ibada na mambo mengine ya heri ikiwa ni utekelezaji wa moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu inayoagiza kufunga mwezi wa Ramadhani, kwani ibada ya Swaumu ni nguzo ya nne.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, lengo kuu la funga ya Ramadhani siyo mtu kushinda njaa na kiu, bali ni kumfanya mfungaji awe Mcha Mungu akijifunza na kuomba toba, kuhurumiana, kusaidiana, kupendana na kujibidiisha katika ibada za kumuomba Mungu msamaha na kutaka fadhila zake kwa yale ambayo wameyatenda kwa siri na dhahiri.

Ndani ya mfungo huo ilishuhudiwa namna waumini walivyokuwa wepesi kuwasaidia wale wasiojiweza, waliwalisha maskini na kujumuika na ndugu, rafiki na majirani zao bila kujali imani kufuturu pamoja hali iliyozidisha upendo baina yao.

Hata hivyo, kipindi hiki kimefikia ukingoni kwani waumini hawa wanauaga rasmi na mwezi huo wa Ramadhani na kuungana na wenzao duniani kote kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitri ambayo huadhimishwa kuashiria kuisha kwa mfungo huo.


Aliyesimama ni Ustadhi Jamal Majuto Shaaban Imam wa msikiti wa Junction Mjini Ngara akitoa Hutuba yake wakati wa Ibada ya Eid el Fitir ,aliyekaa ni Ustadhi Hussein Msema Shekhe wa Mtaa wa Ngara mjini ambapo katika ujumbe wa Eid,pamoja na kufurahia sikukuu ya Eid el Fitri ni vizuri pia Waislamu wakawakumbuka wenye kuhitaji bila kubagua imani zao za kidini kama ambavyo walivyokuwa wakiwasaidia na kutoa misaada kwa yatima, wajane, maskini, wagonjwa na walemavu na wengine bila kujali ni Waislamu na wasio wa Waislamu ili kuendeleza jamii iliyo bora na yenye upendo.


..MNEC wilaya ya Ngara -Issa Samma katikati akiwa na Waumini wengine wakifatilia kile kilichokuwa kinaendelea katika sala ya Eid el Fitir kwenye Viwanja vya Kokoto-Mjini Ngara leo Julai 29,2014.



Aliyesimama ni Ustadhi Jamal Majuto Shaaban Imam wa msikiti wa Junction  na aliyekaa ni Ustadhi Hussein Msema Shekhe wa Mtaa wa Ngara mjini wakati wa ibada hiyo.



Mwenye miwani ni Wajina Mohamed toka TTCL Ngara nae alishiriki sala ya  Eid el Fitiri.

Mmiliki wa Blog hii ya Mwanawamakonda na Mfanyakazi wa Radio Kwizera FM ya Mjini Ngara,Mohamed Ramadhani Makonda aka Mwana wa Makonda akifatilia Hotuba wakati wa Ibada ya  Eid el Fitiri viwanja vya Kokoto Mjini Ngara leo Julai 29,2014.

Toka kulia ni Mdau Saidi Salumu na anaefata ni Ustadhi Yacobo ,Shekhe wa Mtaa wa Junction mjini Ngara,wakitafakari jambo mara baada ya sala ya Eid el Fitiri kumalizika.


Picha juu na chini ni baadhi ya Waumini mbalimbali wa Kiislamu waliojitokeza kushiriki  sala la  Eid el Fitiri viwanja vya Kokoto,mjini Ngara leo Julai 29,2014,ikiwa ni kumaliza siku 30 za Mfungo wa Ramadhani.





UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.

Like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad