AJALI DODOMA:-Taswira ya Basi la MORO BEST Laua watu zaidi ya 10 Papo Hapo Asubuhi ya Leo Julai 30,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 30, 2014

AJALI DODOMA:-Taswira ya Basi la MORO BEST Laua watu zaidi ya 10 Papo Hapo Asubuhi ya Leo Julai 30,2014.


Baadhi ya Miili ya Marehemu muda mchache baada ya kupata ajali kabla ya kupelekwa Hospitalini Kuhifadhiwa...Basi hilo la MORO BEST lilikuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es salaam leo Julai 30,2014.


Baadhi ya Raia/Wasamalia wema wakiokoa majeruhi na kuwaondoa waliofariki ,ambapo idaiwa watu zaidi ya watu 10 wamepoteza maisha.


Hivi ndivyo Basi lilivyo Haribika baada ya Ajali…..Picha na Dodoma yetu Blog

Watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 56 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la MORO BEST, iliyotokea leo Julai 30,2014,majira ya saa mbili asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, Basi hilo limegongana na lori katika eneo la Pandambili, Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma na kwamba miongoni mwa waliofariki ni pamoja na Madereva na Makondakta wa magari yote mawili.

Hata hivyo chazo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kongwa na wengine katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad