Ndege ya Malaysia, Boeing 777 iliyokuwa inatoka Amsterdam kwenda Kula
Lumpur imeanguka Mashariki mwa Ukraine karibu kabisa na mpaka wa Russia, leo,
July 17,2014.
Kwa mujibu wa CNN, waziri wa Malaysia anaehusika na mauala ya
Usafirishaji amesema kuwa abiria 280 na wafanyakazi 15 waliokuwa kwenye ndege
hiyo wamepoteza maisha.
Tweet ya Malaysia Airlines imeeleza kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano
baada ya kutoka Amsterdam.
Kumekuwa na taarifa za awali kuwa ndege hiyo ilipigwa na Ukraine, taarifa ambazo zimekanushwa na Raisi
wa Ukraine.
Rais wa Malaysia ameeleza kupitia twitter jinsi alivyosikitishwa na tukio
hilo na kudai kuwa wataanza uchunguzi wa tukio hilo haraka iwezekanavyo kufahamu
chanzo.
Tukio hili linatokea wakati ambapo bado ndege ya nchi hiyo, Flight 370
iliyopotea March 8, Mwaka huu bado haijapatikana.
|
No comments:
Post a Comment