Jeshi la
polisi limelazimika kumuokoa naibu waziri wa maji Mh Amosi Makala toka katikati
mwa mikono ya makada wa Chadema na CCM katika kata ya Goba mara baada ya diwani
wa viti maalumu CCM wa kata hiyo, alipokuwa akiwatambulisha makada wenzake wa
CCM,kabla ya mkutano huo na wananchi kuvunjika kutokana na vurugu toka kwa
makada wa Chadema na wale CCM.
Akiongea na
waandishi wa habari akiwa ndani ya gari huku likiwa limezungukwa na ulinzi wa
jeshi la polisi na makamanda wa CCM,naibu waziri wa maji amesema kuwa suala la
maji halina itikadi na kuwa amesikitishwa na hatua hii ya kuwa nyima haki
wananchi wengine kusikia sauti ya serikali kutokana an kero hiyo ya maji.
Wakiongea
mara baada ya vurugu hizo mbunge wa jimbo la ubungo mh:john mnyika na
mwenyekiti wa CCM wilya ya Kinondoni bwana Salumu Madenge kwa nyakati tofauti
wameendelea kutupoiana vijembe huku kila mmoja akimalaumu kundi la mwenzake
kuanzisha fujo.
Katika tukio
lisilo kuwa la kawaida naibu waziri ameshuhudia matanki makubwa katika eneo la
Kigogo nyumba mpya yanayo kadiriwa kuwa na ujazo lita laki moja na
therahini,yakiwa yanatumika kuuzia maji kwenye magari ya maji hatua ambayo
inadaiwa kuisababishia hasara ya mabilioni Dawasa na Dawasco.
Ziara hiyo
ya naibu waziri wa maji iliyokuwa imeanzia maeneo ya Makongo juu,Mbezi na Goba
maeneo ambayo yamekuwa hayana mfumo wa maji safi kabla ya ziara hiyi kukatishwa
bila ya kuhutubia wananchi katika eneo la Goba,ambapo licha ya tukio hilo
amesema kuwa kero ya maji itatatuliwa ifikapo September mwaka huu 2014.
Mfuasi wa
CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
|
Mfuasi wa
Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali.
|
Polisi
akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na CHADEMA.
|
Wafuasi
wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara.
|
Wazir Makalla
akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo
la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares
Salaam na Pwani.
|
Mkazi
wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya
Kibamba.
|
Mwalimu wa
Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri
kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo.
|
Askari
akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri
Makalla katika mkutano huo.
|
Wafuasi wa
CCM na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao
wakiwakwenye magari eneo la Kibamba. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
|
No comments:
Post a Comment