Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati
Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana Jijini Dar Es
Salaam kwa Siku mbili kuanzia kesho Ijumaa ya Tarehe 18-19 Julai, 2014, katika
Kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika Siku mbili hizo,Wajumbe wa Kamati Kuu ya
CHADEMA watajadili pamoja na masuala mengine;-
* Mchakato wa Katiba Mpya.
* Taarifa ya hali ya Siasa Nchini.
* Uchaguzi wa ndani ya Chama.
* Taarifa ya fedha, Mpango Kazi na
Bajeti.
* Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba,
Kanuni na miongozo ya Mabaraza ya Chama.
* Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa.
* Taarifa ya Katibu wa Wabunge.
* Rufaa mbalimbali.
* Nembo na Kadi za Mabaraza ya Chama.
Kikao hicho kitatanguliwa na hotuba ya
ufunguzi, ambapo vyombo vya habari vinaalikwa kuhudhuria.
Imetolewa leo Alhamisi, Tarehe 17
Julai, 2014 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya
Habari- CHADEMA.
|
No comments:
Post a Comment