Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa
na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa
habari.
|
Imebainika kuwa
miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji
‘SANGOMA’ ili kupata ujauzito baada ya kukaa muda mrefu
bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo.
Uchunguzi
uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake hao umebaini
kuwa, waume wao wanafanya kazi katika nyadhifa za juu
serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume hao hawajui
kinachoendelea.
Kwa mujibu
wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa,
kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi
wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
Kamanda Kiondo akielezea kuhusu uhalifu wa
Sangoma walionaswa kwa kufanya ngono na wake wa vigogo.
|
Mwanamke
huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini
kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’
ZILISHATUMIKA.
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani ‘kufuli’ za wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.
Kamanda Kiondo akionesha baadhi ya nguo za
ndani, 'kufuli' zilizokutwa kama ushahidi kwa baadhi ya wanawake waliofanyishwa
ngono na sangoma hao.
|
KWA NINI
WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao
ambao hawakupenda majina yao yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua,
walisema ni kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane
hadi 10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
...Kamanda Kiondo akizidi kuonyesha vifaa
vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.
|
Hata hivyo,
baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga
hao.
KAULI YA RPC.
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
........Baadhi ya watuhumiwa wa sakata hilo.
|
Vitu hivyo
viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa
habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda Kiondo.
Waliokamatwa
katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa
pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
...Tunguli zikiteketezwa kwa moto.
|
No comments:
Post a Comment