KOMBE LA DUNIA 2014:-Tazama matokeo ya Ujerumani,Marekani na sare ya Mabingwa wa Africa Nigeria-June 16,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 17, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Tazama matokeo ya Ujerumani,Marekani na sare ya Mabingwa wa Africa Nigeria-June 16,2014.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Nigeria wakiomba dua kabla ya kuanza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Iran katika mchezo wa Kundi F Kombe la Dunia usiku wa June 16,2014 nchini Brazil.

Iran na Nigeria zimetoka 0-0 hapo Jana huko Arena da Baixada Jijini Curitiba Nchini Brazil katika Mechi ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia na hii ndio Droo ya kwanza ya Mashindano haya tangu yaanze June 12,2014.

Nigeria walitawala Mpira lakini walishindwa kuipenya Iran inayofundishwa na Kocha wa zamani wa Manchester United Carlos Queiroz.

Nafasi safi za Nigeria zilikuwa Kipindi cha Kwanza wakati Ogenyi Onazi alipopiga nje na Ahmed Musa kukosa kwa Frikiki.

Na nafasi nzuri ya Iran ilikuwa ile ya Reza Ghoochannejad ambayo iliokolewa na Kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.

Kwenye Mechi nyingine ya Kundi F iliyochezwa (June 15,2014), Argentina iliifunga Bosnia Bao 2-1.

Mechi zinazofuata za Kundi F ni Jumamosi June 21,2014 kwa Argentina v Iran na Nigeria v Bosnia-Herzegovina.

Dejagah wa Iran kushoto akikabiliana na beki wa Nigeria, Joseph Yobo katika mchezo wa Kundi F Kombe la Dunia usiku huu nchini Brazil.




Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza Thomas Muller (kushoto) baada ya kukamilisha hat trick dhidi ya Ureno June 16, 2014 katika ushindi wa bao 4-0 ikiwa ni Mechi ya kwanza kwa Timu zote mbili ambazo zipo Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia 2014.








John Brooks alifunga Bao la Kichwa Dakika 4 kabla Mpira kumalizika na kuipa Timu ya Taifa ya Marekani/USA ushindi wa bao 2-1 kwenye Mechi ya Kundi G iliyochezwa huko Estadio das Dunas Jijini Natal Nchini Brazil. 

USA walitangulia kupata Bao Sekunde ya 29 tu, hili likiwa ni goli la 5 la mapema kwenye Historia ya Kombe la Dunia, alilofunga Clint Demsey, Mchezaji wa zamani wa Fulham.

Andre Ayew aliisawazishia Ghana Dakika ya 82 baada kupokea Pasi ya Kisigino ya Asamoah Gyan.

Mapema Jana(June 16, 2014), kwenye Mechi nyingine ya Kundi G, Germany iliifumua Portugal Bao 4-0.

Thomas Muller  katika mchezo huo alifunga bao 3 katika Dakika ya 12 kwa Penati iliyotolewa baada ya Mario Gotze kuangushwa na Joao Pereira,Mats Hummels alifunga bao la Pili dakika ya 32 na ndipo ikafuatia Kadi Nyekundu katika Dakika ya 37 kwa Pepe ambae alivaana na Muller na Refa kuamua ni Frikiki na yeye kumzonga Mjerumani huyo aliekuwa kakaa chini na kuinamisha kichwa chake kwake kumgusa Mullar kitendo ambacho Refa Milorad Mazic wa Serbia alichukulia kama fujo.

Kabla Haftaimu, Muller tena akapiga Bao na kuifanya Germany 3 Portugal 0 huku Kipindi cha Pili, Thomas Muller akaongeza Bao lake la 3 Dakika ya 78 na Germany kushinda Bao 4-0.

Mechi zinazofuata kwa Kundi G ni Jumamosi June 21,2014, Germany na Ghana na Portugal kucheza na USA Jumapili Juni 22,2014.

Group A
Date Match Result
Thu, 12.06.14 20:00 UTC Brazil : Croatia 3:1 (1:1)
Fri, 13.06.14 16:00 UTC Mexico : Cameroon 1:0 (0:0)
Tue, 17.06.14 19:00 UTC Brazil : Mexico -:- (-:-)
Thu, 19.06.14 22:00 UTC Cameroon : Croatia -:- (-:-)
Mon, 23.06.14 20:00 UTC Cameroon : Brazil -:- (-:-)
Mon, 23.06.14 20:00 UTC Croatia : Mexico -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Brazil 1 1 0 0 3:1 2 3
2 Mexico 1 1 0 0 1:0 1 3
3 Cameroon 1 0 0 1 0:1 -1 0
4 Croatia 1 0 0 1 1:3 -2 0
Group B
Date Match Result
Fri, 13.06.14 19:00 UTC Spain : Netherlands 1:5 (1:1)
Sat, 14.06.14 22:00 UTC Chile : Australia 3:1 (2:1)
Wed, 18.06.14 16:00 UTC Australia : Netherlands -:- (-:-)
Wed, 18.06.14 19:00 UTC Spain : Chile -:- (-:-)
Mon, 23.06.14 16:00 UTC Australia : Spain -:- (-:-)
Mon, 23.06.14 16:00 UTC Netherlands : Chile -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Netherlands 1 1 0 0 5:1 4 3
2 Chile 1 1 0 0 3:1 2 3
3 Australia 1 0 0 1 1:3 -2 0
4 Spain 1 0 0 1 1:5 -4 0
Group C
Date Match Result
Sat, 14.06.14 16:00 UTC Colombia : Greece 3:0 (1:0)
Sun, 15.06.14 01:00 UTC Ivory Coast : Japan 2:1 (0:1)
Thu, 19.06.14 16:00 UTC Colombia : Ivory Coast -:- (-:-)
Fri, 20.06.14 22:00 UTC Japan : Greece -:- (-:-)
Tue, 24.06.14 20:00 UTC Japan : Colombia -:- (-:-)
Tue, 24.06.14 20:00 UTC Greece : Ivory Coast -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Colombia 1 1 0 0 3:0 3 3
2 Ivory Coast 1 1 0 0 2:1 1 3
3 Japan 1 0 0 1 1:2 -1 0
4 Greece 1 0 0 1 0:3 -3 0
Group D
Date Match Result
Sat, 14.06.14 19:00 UTC Uruguay : Costa Rica 1:3 (1:0)
Sun, 15.06.14 22:00 UTC England : Italy 1:2 (1:1)
Thu, 19.06.14 19:00 UTC Uruguay : England -:- (-:-)
Fri, 20.06.14 16:00 UTC Italy : Costa Rica -:- (-:-)
Tue, 24.06.14 16:00 UTC Italy : Uruguay -:- (-:-)
Tue, 24.06.14 16:00 UTC Costa Rica : England -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Costa Rica 1 1 0 0 3:1 2 3
2 Italy 1 1 0 0 2:1 1 3
3 England 1 0 0 1 1:2 -1 0
4 Uruguay 1 0 0 1 1:3 -2 0
Group E
Date Match Result
Sun, 15.06.14 16:00 UTC Switzerland : Ecuador 2:1 (0:1)
Sun, 15.06.14 19:00 UTC France : Honduras 3:0 (1:0)
Fri, 20.06.14 19:00 UTC Switzerland : France -:- (-:-)
Sat, 21.06.14 22:00 UTC Honduras : Ecuador -:- (-:-)
Wed, 25.06.14 20:00 UTC Honduras : Switzerland -:- (-:-)
Wed, 25.06.14 20:00 UTC Ecuador : France -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 France 1 1 0 0 3:0 3 3
2 Switzerland 1 1 0 0 2:1 1 3
3 Ecuador 1 0 0 1 1:2 -1 0
4 Honduras 1 0 0 1 0:3 -3 0
Group F
Date Match Result
Mon, 16.06.14 22:00 UTC Argentina : Bosnia and Herzegovina 2:1 (1:0)
Mon, 16.06.14 19:00 UTC Iran : Nigeria 0:0 (0:0)
Sat, 21.06.14 16:00 UTC Argentina : Iran -:- (-:-)
Sun, 22.06.14 22:00 UTC Nigeria : Bosnia and Herzegovina -:- (-:-)
Wed, 25.06.14 16:00 UTC Nigeria : Argentina -:- (-:-)
Wed, 25.06.14 16:00 UTC Bosnia and Herzegovina : Iran -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Argentina 1 1 0 0 2:1 1 3
2 Iran 1 0 1 0 0:0 0 1
2 Nigeria 1 0 1 0 0:0 0 1
4 Bosnia and Herzegovina 1 0 0 1 1:2 -1 0
Group G
Date Match Result
Mon, 16.06.14 16:00 UTC Germany : Portugal 4:0 (3:0)
Tue, 17.06.14 22:00 UTC Ghana : USA 1:2 (0:1)
Sat, 21.06.14 19:00 UTC Germany : Ghana -:- (-:-)
Mon, 23.06.14 22:00 UTC USA : Portugal -:- (-:-)
Thu, 26.06.14 16:00 UTC USA : Germany -:- (-:-)
Thu, 26.06.14 16:00 UTC Portugal : Ghana -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Germany 1 1 0 0 4:0 4 3
2 USA 1 1 0 0 2:1 1 3
3 Ghana 1 0 0 1 1:2 -1 0
4 Portugal 1 0 0 1 0:4 -4 0
Group H
Date Match Result
Tue, 17.06.14 16:00 UTC Belgium : Algeria -:- (-:-)
Wed, 18.06.14 22:00 UTC Russia : South Korea -:- (-:-)
Sun, 22.06.14 16:00 UTC Belgium : Russia -:- (-:-)
Sun, 22.06.14 19:00 UTC South Korea : Algeria -:- (-:-)
Thu, 26.06.14 20:00 UTC Algeria : Russia -:- (-:-)
Thu, 26.06.14 20:00 UTC South Korea : Belgium -:- (-:-)
Position Team P W D L GS GD Points
1 Algeria 0 0 0 0 0:0 0 0
1 Belgium 0 0 0 0 0:0 0 0
1 Russia 0 0 0 0 0:0 0 0
1 South Korea 0 0 0 0 0:0 0 0

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad