KOMBE LA DUNIA 2014:-Tazama Kipa wa Mexico alivyowazuia Wenyeji Brazil na kutoka Sare…Pia Ratiba na Matokeo Mengine ya Mechi za June 17,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 18, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Tazama Kipa wa Mexico alivyowazuia Wenyeji Brazil na kutoka Sare…Pia Ratiba na Matokeo Mengine ya Mechi za June 17,2014.

Wakati wa mchezo huo June 17,2014,Usiku ulikuwa vuta ni kuvute ingawa Neymar alikosa Bao la Kichwa ambacho Kipa Ochoa wa Mexico aliokoa vizuri, Kipindi cha Pili Brazil, hasa mwishoni, walikuja juu mno na kukosa Bao kadhaa huku Kipa Ochoa akiokoa tena na tena na, bila shaka, ndie alieinusuru Mexico.

Mechi za Pili kwa Kundi A la Fainali za Kombe la Dunia zimeanza jana June 17,2014, Estadio Castelão, Fortaleza na Wenyeji Brazil kutoka Sare ya 0-0.

Sare hii imeibakisha Brazil juu kwenye Kundi wakiwa na Pointi 4 sawa na Mexico.
Jumatano June 18, 2014,ni zamu ya Cameroon na Croatia kucheza Mechi zao za Pili za Kundi A baada ya wote kupoteza Mechi zao za kwanza.

Mechi ya mwisho Brazil watacheza na Cameroon huko Nacional, Brasilia Jumatatu June 23,2014 na wakati huo huo Mexico kuivaa Croatia.

Neymar akijaribu kuwatoka mabeki wa Mexico katika mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana.


MSIMAMO.

KUNDI A
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Brazil
2
1
1
0
3
1
2
4
Mexico
2
1
1
0
1
0
1
4
Cameroon
1
0
0
1
0
1
-1
0
Croatia
1
0
0
1
1
3
-2
0
Timu ya Taifa ya Ubelgiji walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Algeria Bao 2-1 kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia iliyochezwa jana June 17,2014 huko Estadio Mineirão, Belo Horizonte, Brazil.
 Algeria walipata Bao lao kwa Penati ya Dakika ya 24 iliyofungwa na Sofiane Feghouli, anaechezea Klabu ya Valencia huko Spain, Penati iliyotolewa baada ya yeye mwenyewe kuchezewa Faulo na Jan Vertonghen anaecheza huko England na Klabu ya Tottenham.


Hadi Mapumziko, Algeria walikuwa wakiongoza Bao 1-0.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 70, Kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini, alisawazisha kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Kevin De Bruyne anaecheza Bundesliga na VfL Wolfsburg.

Bao la ushindi la Ubelgiji lilifungwa na Dries Mertens wa Napoli ya Italy baada ya kaunta-ataki ambapo alipokea pasi safi toka kwa Eden Hazard wa Chelsea.



Fellaini kulia akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Ubelgiji bao la kwanza katika ushindi wa timu yake wa 2-1.
JUMATANO, JUNI 18, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Australia v Netherlands
B
Estadio Beira-Rio
2200
Spain v Chile
B
Estadio do Maracanã
0100
Cameroon v Croatia
A
Arena Amazonia
ALHAMISI, JUNI 19, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Colombia v Ivory Coast
C
Nacional
2200
Uruguay v England
D
Arena Corinthians
0100
Japan v Greece
C
Estadio das Dunas



Mechi ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia iliyochezwa Arena Pantanal, Cuiba kati ya Russia na South Korea ilimalizika kwa Droo ya 1-1.

South Korea walitangulia kufunga katika Dakika ya 68 kwa Bao la Lee Keun-ho na Mapema Jana June 17,2014, kwenye Mechi ya kwanza ya Kundi F, Belgium iliifunga Algeria 2-1.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad