 |
Mchezaji Oribe Peralta (kushoto) akiifungia bao
pekee la ushindi kwa Mexico walipopambana na Cameroon June 13, 2014, katika Fainali za
Kombe la Dunia 2014-Nchini Brazil.
|
Goli pekee la Oribe Peralta
dakika ya 61 ya Mchezo limeipa mwanzo mzuri Timu ya Taifa ya Mexico katika
Fainali za Kombe la Dunia 2014,baada ya kuilaza 1-0 Cameroon katika mchezo wa
Kundi A wa fainali hizo June 13, 2014,
jioni hii Uwanja wa Dunas mjini Natal.
Katika mchezo huo,Refa wa
Colombia, Wilmar Roldan alikataa mabao mawili ya Mexico akida mfungaji,
mshambuliaji wa zamani wa Spurs, Giovani dos Santos alikuwa ameotea.
Matokeo hayo yanaiweka Mexico katika mazingira mazuri
ya kufuzu sambamba na vinara wa kundi hilo, wenyeji Brazil ambao watamenyana
nao Jumanne mjini Fortaleza.
Group A
Group B
Group C
Group D
Group E
Group F
Group G
Group H
No comments:
Post a Comment