Wajumbe wa Baraza kuu la
Chadema June 23 2014 walikua na mkutano mkuu wa chama hicho kwa umma ambao
ulihusisha waandishi mbalimbali wa habari wakiwa zaidi ya 80.
|
Athumani H. Balozi ambaye ni
Katibu Mkuu wa Chadema mkoa wa Tabora ndiye aliyesoma taarifa hiyo kwa niaba ya
Wajumbe wote akianza kwa kusema>>’Sisi ni wajumbe wa Baraza Kuu na
mkutano mkuu wa Chama ambapo pamoja nasi tumejumuika na wenyeviti wa mabaraza
ya WANAWAKE WA MIKOA YA TABORA NA SINGIDA, MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TABORA
pamoja na MUASISI WA CHADEMA kutokea mkoa wa SINGIDA na mwenyekiti wa M4C
wilaya ya SINGIDA hivyo tunafanya jumla ya tuliokutana kwa jambo hili kuwa ni
wanachadema 82’
Kuwaeleza namna ambavyo
tumekuwa tukisononeshwa na mwenendo wa chama chetu kwa kipindi kirefu sasa,
hivyo tunaomba mtusaidie kuufikishia umma mawazo ya wanachadema
tunaowawakilisha huko mikoani tutokapo’
Sababu nyingine waliyosema ni
kushindwa kwa uongozi wa kitaifa ambao haya ni maelezo yao>>’Tunasikitika
kuona kwamba kadri siku zinavyoenda Uongozi wa juu wa chama unazidi kushindwa
kufanya kazi ya kukiimarisha chama’
‘Baada ya jitihada
tulizozifanya kwenye uchaguzi wa 2010 sehemu mbali mbali, ni dhahiri ushindani
kwa sasa ungekuwa mkubwa sana kiasi cha chama kushika dola uchaguzi ujao iwapo
chama kingejikita kwenye jitihada za ujenzi wa chama’
‘Badala yake uongozi wetu
umewasaliti Watanzania waliokuwa na tumaini kubwa sana na chadema na kuwekeza
nguvu nyingi sana kwenye Kuimarisha migogoro baina ya viongozi wakuu wenyewe
kwa wenyewe, wanaimarisha ubinafsi miongoni mwa wanachama, wanaimarisha Udini
na Ukabila pamoja na ubadhilifu wa mali za chama’
‘Matendo haya ya viongozi
wetu ni UNAFIKI wa kisiasa, kiasi cha kutumia mabilioni ya shilingi kwenda
kumshambulia ama kummaliza kisiasa kiongozi mwenzao (Zitto Kabwe) na kuacha
ujenzi wa chama ukiendelea kuporomoka’
‘Kwenye ujinga huu, hakuna wa
kumlaumu zaidi ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na na Katibu Mkuu Dkt.Wilbrod
Slaa.
Hawa wanafaa sasa kuhukumiwa na watanzania wanaopenda mabadiliko ya kweli
kwa kurudisha nyuma jitihada za kuwakomboa na kukiimarisha chama na badala yake
wamekuwa wakitumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi za chama kujiimarisha wao
wenyewe’
Sehemu nyingine ambayo
waliigusia ni kuhusu walichosema ni ubadhilifu wa fedha na mali za Chama ambapo
hapa pia wamesema>>’Mtakumbuka kwamba baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka
2010 ruzuku ya chama iliongezeka kutoka million 56 mpaka milioni 239 kwa mwezi’
‘Tunasikitika kuona kwamba
mpaka sasa chama kimeshindwa kufanya uwekezaji wenye tija ili kukisaidia chama
kiweze kujiendesha bila kutegemea Ruzuku ama kukopa kutoka kwa Mbowe kama
mwenyewe anavyopenda tuwe tunafanya’
‘Mpaka sasa chama kimepokea
jumla ya shilingi BILIONI 10.038 kama ruzuku kutoka serikalini ili chama
kijiendeshe.
Ni narudia, mpaka sasa chama kimepokea kutoka serikalini jumla ya
SHILINGI BILLION KUMI, NA MILIONI THELASINI NA NANE’
‘Cha kusikitisha kwa kipindi
chote hicho na kiasi chote hicho cha pesa zitokanazo na kodi za waTatanzania
pesa ambazo zinasababishwa na kazi kubwa tuliyoifanya ya kukipigania chama
kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, leo chama hakina hata jengo moja la OFISI MIKOANI
KOTE na OFISI zote za mikoa tunapanga kwenye FREMU za maduka na hata Pango la
fremu hizo tunajilipia wenyewe kwa kuchangishana, Mbowe na Slaa wanatumia
MABILIONI HAYA KURUKA NA CHOPA sisi huku chini tunaendelea kumenyeka kwa kigezo
cha UKAMANDA ,huu ni utumiaji mbaya wa mali za chama’
‘Tunasikitishwa sana na
kitendo cham mwenyekiti MBOWE kusema anajilipa madeni aliyokikopesha chama kila
siku, kiasi cha zaidi ya MILLIONI 700 Mbowe anajilipa kama madeni aliyokikopesha
chama. Sasa tunashindwa kuelewa deni hili ni deni gani lisiloisha?, na je deni
hili alikikopesha chama kwa mkataba gani?, na aliusaini mbele ya nani huo
mkataba wa mkopo?, Taratibu za chama kukopa zipo wazi je zilifuatwa?. Haya ni
matumizi mabaya ya fedha za umma’
‘Tunasikitishwa na kitendo
cha mwenyekiti mbowe kukiuzia chama MAGARI CHAKAVU kwa zaidi ya million 600,
Huku akijua ni chakavu na kwamba kabla ya kukiuzia chama alikuwa anakikodisha
magari hayo’
‘Masikitiko yetu ni kitendo
cha MBOWE kununua LANDCRUISER V8 VX 2 kwa pesa za chama na kasha kuja kukiuzia
chama, lakini kama haitoshi mpaka leo hii Gari hizo zimesajiriwa kwa majina ya
MBOWE HOTELS. Haya ni matumizi mabovu mno ya mali za umma na kwamba yampasa
sasa ajitathmini kama anapaswa kuendelea kuwa kiongozi mtetezi wa wanyonge ama
mnyonyaji wa wanyonge’
‘Tunahudhunishwa na kitendo
cha Dkt. SLAA kutufanyia huduma ya kutuuzia ukombozi, haiwezekani kwa akili ya
kawaida, ukawa katibu mkuu unayelipwa zaidi ya million 130 kwa mwaka na chama
halafu makatibu na viongozi wako wa mikoani wanalipwa 0 kwa mwaka. Huu ni
udalali na unafiki wa kisiasa’
‘Ingawa kuna vitu vingi
wamevizungumza lakini hii nyingine ni Uvunjifu wa katiba na kanuni za chama
ambapo wamesema>>’Mpaka sasa viongozi wakuu hawa, wamevunja katiba ya
chama kwa mambo makuu matatu yafuatayo’
- 1. Kitendo cha kutoka na kususia kwenye Bunge la katiba bila kuruhusiwa na vikao halali vya chama.
- 2. Bunge la katiba lilikuwa ni mazao ya Juhudi zetu sisi wanaCHADEMA tuliopambana nchi nzima kuidai katiba.
‘Chama chetu kilikuwa na
fursa kubwa ya kutuwakilisha kwenye kuandika katiba hiyo na kufanya marekebisho
makubwa kwa kadri tulivyoazimia,Lakini kususa Bunge la katiba lililotokana na
Sheria mliyoishiriki kuitunga, ni kutufanya sisi sote tunaowakilishwa na
viongozi hawa tuonekane ni majuha’
Kwa kuwa CHADEMA ni miongoni
mwa waasisi wa mchakato huu wa Katiba. Ni kuwasaliti Watanzania na kuikosesha
nchi fursa ya kuandika katiba kususa.
- 2. Kitendo cha Kuunda Baraza Kivuli la mseto na vyama tulivyowaaminisha watanzania kuwa vina ushirika na CCM.
‘Kwenye hili, chama kinapaswa
kuelezwa kama mazingira yaliyowafanya wenzetu hawa kuungana na CCM yamebadilika
ama bado yapo?, Chama kinapaswa kuelezwa na mbowe na Slaa kuwa Uteuzi wa Mbatia
kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais wa CCM umebatilishwa ama la?’
‘Lakini chama pia kitueleze
kama Nafasi ya juu ya viongozi wa CUF kwenye serikali ya mseto na CCM kule
Zanzibar haipo tena. Vinginevyo viongozi wetu wote walioshiriki hili wanatakiwa
wawajibike haraka iwezekanavyo’
- 3. Kutokuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu. Katiba yetu inatuagiza Kuwa Baraza kuu la chama litaitishwa kila baada ya miezi kumi na mbili. Kwa kuwa baraza kuu la mwisho liliitishwa February 2013, kulipaswa kuitishwa tena baraza kuu lingine kabla ya mwezi February 2014 kuisha.
‘Baada ya kukamilika kwa
maelezo yao wametoa agizo lao ambalo wamesema>>’Tunawaagiza viongozi wetu
waitishe haraka MKUTANO WA BARAZA KUU ili pamoja na mambo mengine viongozi wetu
wajieleze mbele ya Wajumbe ni kwanini Tusiwachukulie hatua za kinidhamu kwa
makosa ya UBADHILIFU, KUSALITI NDOTO ZA WATANZANIA, na KUHAMASISHA MGAWANYIKO
NA UBAGUZI NDANI YA CHAMA’
• MBOWE na Dkt. SLAA wanatakiwa wajipime wenyewe kama ni sahihi
chama kukodi HELKOPTA (CHOPA) 3 na kutumia zaidi ya BILIONI 1.4 za ruzuku ambazo
ni kodi za Watanzania halafu eti tunashinda KATA TATU kati ya zaidi ya KATA 27,
Yaani kila HELKOPTA MOJA imeleta KATA MOJA ama kila SHILINGI MILLIONI 466.6 kwa
KATA MOJA, halafu chama hakionyeshi kushtuka wala Kujali
MBOWE na Dkt. SLAA wajipime
zaidi kama wanafaa kuendelea kuwa viongozi wa chama huku chama kikizidi
kudidimia kila uchao kiasi cha KUDHARIRISHWA KWA kupata KURA 2000 CHALINZE na
KURA 5000 KALENGA huku chama kikitumia zaidi ya MILLIONI 600 kushiriki CHAGUZI
HIZO’.
Habari Na:-millardayo.com
No comments:
Post a Comment